Monday, 4 June 2012

WASIFU WA KOCHA DI MATTEO


Roberto Di Matteo, amezaliwa 29 Mei 1970. Ni mwanasoka wa zamani kutoka nchini Itali na ndiye kocha wa mpito wa timu ya Chelsea kwa msimu ulioishia mwaka 2012. Kipindi anacheza soka, alicheza kama kiungo katika klabu ya Uswiss Schaffhausen, Zurich na Aarau kabla ya kujiunga na klabu ya Lazio na Chelsea ya Uingereza. Aliichezea timu ya Italy mara 34, akifunga jumla ya magoli mawili, alicheza kwenye kombe la Euro mwaka 1996 na Kombe la dunia 1998.
Alistaafu kama mchezaji Februari 2002 akiwa na umri wa miaka 31, baada ya kuandamwa na matatizo ya majeruhi. Tangu hapo amekuwa akiziongoza kama kocha timu, Milton Keynes Dons, West Bromwich Albion na Chelsea. Akiwa kama kocha wa Chelsea amefanikiwa kushinda kombe la FA 2012 na kombe la klabu bingwa UEFA, ikiwa ndio ushindi wa mara ya kwanza kwa timu hiyo ya Chelsea.

Switzerland na Lazio
Amezaliwa Uswis, Wazazi wake ni raia wa Itali kutoka mji wa Paglieta, Abruzzo, Di Matteo alinza safari yake ya soka kwa kuichezea klabu ya Uswis Schaffhausen, kabla ya kujiunga na klabu ya Aarau mwaka 1991. Alitwaa ubwinga wa Nationalliga A, akiwa na klabu ya Aaru mwaka 1993.Ligi hiyo ikiwa ni ligi ya 14 kwa ubora barani Ulaya kwa mujibu wa UEFA. Katika kipindi hicho hicho alifanikiwa kujinyakulia tuzo ya uchezaji bora wa mwaka, Mwaka 1993 alisaini uhamisho bure  kipindi cha majira ya joto na kuelekea kuelekea klabu ya Lazio. Di Matteo alitokea kuchezea timu ya Lazio mara kwa mara na ndipo alipoanza kutokea  kwenye kikosi cha Timu yake ya Taifa ya Itali kipindi anachezea klabu yake ya jijini Roma.
Hata hivyo mfarakano baina yake na kocha wake Zdeněk Zeman, baada ya kosa la kiulinzi lililopelekea kufungwa na timu ya Internazionale, ulimaliza safari yake na timu ya Lazio, matokeo yake akasainiwa na Ruud Gullit wa Klabu ya Uingereza kwa dau lilioweka rekodi ya £ 4.9 milioni.

Chelsea
Di Matteo alifunga goli la ushindi dhidi ya Middlesbrough katika mchezo wa nyumbani akiwa na klabu yake ya Chelsea katika mchezo wake wa kwanza.Uwezo wake wa kutoa pasi zenye uwezo wa hali ya juu na mashuti ya mbali yenye usahihi, ulimfanya awe ni mmoja wa wachezaji wenye uwezo na msukumo wa hali ya juu wa klabu yake ya Chelsea mwishoni mwa miaka ya tisini. Alichangia magoli tisa. Ikiwemo misaada ya umbali mrefu dhidi ya Tottenham Hotspur na Wimbledon. Aliisaidia Klabu yake kumaliza ligi ikiwa ya sita katika msimamo wa ligi, ikipata mafanikio ya hali ya juu tangu msimu wa mwaka 1989-1990, nakufanikiwa kufika katika fainali la kombe la FA mwaka 1997 Wembley. Mara tu baada mchezo huo kuanza ndani ya sekunde 42 alifunga goli dhidi ya Middlesbrough, Di Matteo alifunga goli la ufunguzi umbali wa yadi 30 na Chelsea kushinda 2-0.goli la Dimatteo ndio lilikuwa goli lililowahi kufungwa mapema zaidi hadi rekodi hiyo ilipovunjwa mwaka 2009 na Louis Saha wa Everton.
Msimu uliofata Di Matteo aliendelea kudhihirisha thamani yake kwa timu yake, kwa kupachika magoli kumi na kutoa  misaada ya hapa na pale, na Chelsea kuelekea kudai Footbal League Cup and na Winners Cup. Na kujipatia heshima ya Baralni  ulaya kwa mara nyingine tangu mwaka 1971 kwa kushinda dhidi ya Middlesbrough, Di M\tteo alifunga goli la pili, Di Matteo alicheza kati kama kiungo akiwa pembeni ya Gustavo Povet, Dennis Wise na Dan patrescu katika msimu wa mwaka 1998-99 ambapo Chelsea ilimaliza wa tatu

Katika msimu wa mwaka 1999-2000 Di Matteo alitolewa kikosini kutokana na majeraha ila aliridu mwishoni mwa msimu na kufunga magoli muhimu, likiwemo goli lake la tatu la ushindi ndani ya Wembley kwa mara nyingine katika kombe la FA, katika mchezo mgumu Di Matteo alitumia nafasi vizuri iliotokana na kosa lililofanywa na kipa wa Aston Villa David James katika dakika ya 71 na kujipatia goli la ushindi, na kuwazawadia Chelsea kwa mara nne katika kipindi cha miaka mitatu. Hii ilimfanya Di Matteo Aseme” ni aibu kuona wanauteketeza , umekuwa ni uwanja wenye bahati sana kwangu”

Mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2000 na 2001, alijikuta akivunjika mguu mara tatu katika kombe la UEFA dhidi ya St gallen klabu ya Uswisi na kutocheza kwa miezi 18 iliofata. Februari 2002 alitupilia mbali matumaini ya kurudi kucheza akitoka kwenye majeruhi aliyoyapata na kustaafu katika umri wa miaka 31.
“kama shukrani ya mchango kutoka kwa kiungo uliochangia mabadiliko ya klabu” kocha wa kipindi hicho Claudio Ranieri alimpa heshima ya kukiongoza kikosi cha Chelsea  katika fainali za kombe la FA 2002, ambapo ilipoteza dhidi ya Arsenal kwa 2-0.
Di Matteo alichaguliwa kama mchezaji wa Kihistoria wa klabu ya Chelsea. Katika miaka sita alipokuwa Chelsea aliichezea Chelsea mara 175 nakushinda magoli 26, hakuwahi  kupoteza uwanjani Old Trafford

Kimataifa

Di Matteo alitokea katika kikosi cha timu ya Itali kwa mara ya kwanza 16 Novemba 1994 ndani ya uwanja wa Stadio La Favorita, Palermo, Sicily. Aliingia uwanjani dakika ya 55 kama mbadala wa Demetro Albertinias, Itali ilipoteza 2-1 dhidi ya Croatia katika mechi za kufuzu Euro 1996.Alianza mwanzoni mwa mchezo katika mchezo wake wa pili katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Uturuki tarehe 21 Desemba 1994 katika uwanja wa Stadio Adriatico ndani Pescara. Ambapo ilishinda 3-1. Aliendelea kucheza timu yake ya Itali katika ngazi ya makundi 1996 dhidi ya Urusi na Ujerumani

Goli lake la kwanza alifunga kwenye mchezo wake wa 23 akiwa na timu yake ya taifa, katika michezo ya kufuzu kombe la Dunia la mwaka 1998 mnamo 30 April 1997, Itali ilishinda 3-0 dhidi ya Poland.Di matteo.DI Matteo alifunga goli moja la ziada, dhidi ya Slovakia Januari 1998. Alikuwemo kwenye kikosi cha kombe la dunia la mwaka 1998 na kuchezea michezo miwili ya ngazi ya makundi dhidi ya Chile na Cameroon. Mechi dhidi ya Cameroon Montpeller ndiyo uliokuwa mchezo wake wa mwisho kuichezea timu yake ya Itali.

Akiwa kama Kocha wa Chelsea

Baada ya kushindwa kufanikiwa kuwa meneja wa timu ya Birmingham City. Di Matteo aliteuliwa kuwa kocha msaidizi wa André Villas-Boas (kocha mpya wa Chelsea 29 Juni 2011).
Baada ya kufukuzwa kazi kocha André Villas-Boas, Di Matteo alipewa madaraka ya mpito na kuiongoza timu ya Chelsea kuanzia March 2012.Aliendelea kutambulika kama kocha wa mpito kwa mujibu wa klabu ya Chelsea. Alianza kupata mafanikio ya moja kwa moja mara tuu baada ya kupewa timu, alishinda dhidi ya Birmingham City, katika mzunguko wa tano wa kombe la FA, Stoke city katika ligi ya Uingereza na Napoli katika mzunguko wa 16 kombe la Klabu bingwa UEFA nakushinda 4-1 baada ya mechi ya kwanza Chelsea kupoteza 3-1, walipokuwa chini ya uongozi wa André Villas-Boas
Di Matteo alishinda dhidi ya Tottenham kwenye nusu fainali za kombe la FA na Dhidi ya Benfica kwenye robo fainali ya UEFA, tarehe 24 April  aliipatishia Chelsea ushindi dhidi ya Barceloma kwenye nusufainali kwa jumla ushindi wa 3-2 nyumbani na  ugenini, na kuwa toa barcelona waliokuwa wakitetea ubingwa wa klabu bingwa UEFA, Mei 5 Chelsea ilishinda dhidi ya Liverpool 2-1 kwenye mchezo wa fainali wa kombe la FA ndani ya uwanja wa wembley.

19 Mei Di Matteo aliingoza Chelsea nakushindaUEFA kwa kuishinda klabu ya Ujerumani Bayern Munich, ushindi mnono ulipatikana kwa penati, na kuifanya Chelsea kushinda kombe la UEFA kwa mara ya kwanza na kuifanya ifuzu katika msimu wa klabu bingwa ulaya wa 2012-2013, baada ya kuto maliza miongoni mwa timu nne ambazo zingesonga mbele, hii ikapelekea pelekea kutolewa kwa wapinzani wao wa jijini  London Tottenham Hotspur kutofuzu katika kinyanganyoro hicho cha UEFA.
Maisha yake ya Kifamilia
Di Matteo ameo na ana watoto wa tatu, na kwa sasa hv anaishi Leamington Spa, Warwickshire



No comments:

Post a Comment