Sunday, 3 June 2012

Wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani Tiger Woods na Kobe Bryant.


Toleo la mwaka 2011 May 31

Mafanikio ya mwanamichezo Tiger Woods, imekuwa ikidorora kwa kipindi cha miaka miwili iliopita. Wadhamini wakubwa kama Accenture, AT&T, Gillette na PepsiCo wamejitoa katika udhamini. Tangu November mwaka jana,pindi tu tukio la ajali ya gari lilipojitokeza na muendelezo wa kashfa zilizofata.

Biashara yake ya kudizain viwanja vya golf nayo iliporomoka kifaida kutoka na mporomoko wa hali ya uchumi duniani.Na nuksi ya muendelezo wa kutoshinda kwenye vinyanganyiro vya mashindano ya golf  kwa kipindi cha miezi 20 na ushee, imepelekea gwiji huyo aliyekuwa mwanamichezo namba moja katika michezo ya golf kuwa wa 13 duniani, na mapato yake ya kipungua kwa dola milioni 50, kwa kipindi cha miaka 2 miwili iliyopita.

Pamoja na yote hayo Tiger Woods bado ndiye mwanamichezo namba moja ulimwenguni kwa kulipwa pesa nyingi, na hakuna anayemkaribia kwa karibu, Akipata dola za kimarekani milioni 75 kwa kipindi cha miezi 12 iliopita, akimuacha kwa mbali sana Kobe Bryant aliyejitengezea dola milioni 53 za kimarekani katika msimu huo huo.

Mafanikio yake kwa zaidi ya asilimia hamsini yametokana na wadau wake wa muda mrefu Kampuni ya Nike na Electronic Arts, ambao wote hawa waliingia naye mkataba kuanzia mnamo mwaka 1998 akipokuwa rasmi mwanamichezo professional,

Kwa mara nyingine tena wanamichezo wa kike, wakiwa nyuma katika takwimu hizi za wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani.Mcheza Tennis Mara Sharapova ndiye mwanamke pekee aliyeweza kupenya katika orodha ya wanamichezo 50 wanaolipwa zaidi duniani, ni wa 29 akijipatia dola milioni 24.2, kwa kiasi kikubwa kutoka kwa wadau wake kama Nike.


HABARI HII NI TOLEO LA MWAKA JANA TAREHE 31 MAY 2011, KWA MUJIBU WA TAKWIMU ZA FORBES


No comments:

Post a Comment