Friday, 15 June 2012

SITE UNDER REVIEW STAY TUNED/MTANDAO UNAFANYIWA MAPITIO ENDELEA KUFATILIA

Wednesday, 6 June 2012

Proff Jize akipafom kwenye show : DAR LIVE


Picha kwa Hisani ya National Geographic Channel

Child Portrait kwa hisani ya National Geographic Channel


Arctic skuas, also called parasitic jaegers, have a well-earned reputation as avian pirates, stealing much of their food from other birds.

Mabilionea Vijana Duniani


Mabilionea wanne vijana wanahusika moja kwa moja na facebook, wawili ni watoto wa aliyekuwa Waziri mkuu wa Lebanon Hayati Rafic Hariri, na mmoja ni mwananke. Wafuatao ni mabilionea  vijana kwa mujibu wa mtandao wa peekyou.com

1. Mark Zuckerberg
Mark Zuckerberg ambaye sasa anaumri wa miaka 28, alizindua facebook kwenye bweni lake kipindi anasoma chuo na amekuwa huku akizungukwa na wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa duniani. Utajiri umeongezeka kwa kasi baada ya kuiorodhesha facebook kwenye soko la hisa, anathamani ya dola bilioni 15 kwa mujibu wa takwimu. Ndiye anaengoza katika orodha ya mabilionea vijana.

2. Scott Duncan
Sasa akikaribia umri wa umri wa miaka 30, amejipatia utajri wake kwa kuridhi mali kutoka kwa marehemu mzee wake, ambaye alianzisha kampuni ya Energy. Anasadikika kuwa na thamani ya dola bilioni 4 za kimarekani

3. Dustin Moskovitz
Moskovitz alifahamina na Mark tangu wapo chuoni, alifanya kazi Facebook kipindi  cha awali cha ukuaji wa kampuni ya facebook, Hivi karibuni ameamua kujihusisha na michakato mingine ikiwemo na shuhuli za misaada, kwa mujibu wa forbes anathamani ya dola bilioni 3.5



4.Sean Parker
Muanzilishi wa Kampuni ya Napster na raisi wa kwanza wa Facebook anathamani ya zaidi dola bilioni mbili. Parker mwenye umri wa miaka 32, amekuwa mshauri mkuu wa zuckerberg na ndiye anayefahamika zaidi kwa kumshauri Mark kubadilisha jina la kampuni ya facebook kutoka kwenye kuitwa “ the facebook” hadi “facebook”. Na ndiye aliyekuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kuwekeza kwenye mtandao wa muziki wa Spotify

5. Eduardo Saverin
Ni mwanzilishi mwenza wa facebook ambaye sasa anamakadirio wa utajiri wenye thamani ya dola bilioni 2, ila ilimlazimu kupigania hadhi yake hiyo, aliishitaki kampuni ya facebook, yalifanyika maelewano nje ya mahakama. Kama ilivyo wasilishwa kwenye filamu ya "The social Network", Saverin mwenye umri wa miaka 30, amekulia kwenye familia ya kitajiri anafahamika kama mpenda kula  bata.

Wengineo ni pamoja na ...
Fahdi Hariri
Robert Pera
Ayman Hariri
Yang Huiyan
Albert Von Thurn Und Taxis

Tweet kutoka kampuni ya Asus iliozua Utata


 Ni ujumbe wa twita, uliozua mijadala kwenye mitandao ya intaneti kwa kushutumiwa kuwa unamdhalilisha mwanamke. Kampuni ya Electronics Asus iliufuta ujumbe wake huo ulioambatanishwa na picha inayomuonyesha mwanamke akielezea bidhaa mpya ya kampuni hiyo mara tu baada malalamiko kuanza.
Ni picha iliopigwa kwa kuuchukua upande wa nyuma ya mwili wa mrembo huyo ikiambatana na ujumbe unaosema “ picha ya nyuma ni nzuri sana,  kama ilivyo Transformer AIO”
Posti hiyo ilipotea kwa haraka sana, ila walichelewa kwani ilishadakwa na watu kuanza kuichangia na wenzao, na kusambaa kwa kasi kwenye mitandao mingine na  malalamiko na shutuma kuanza kuelekezwa kwa kampuni hiyo.hata hivyo kampuni ya Asus iliomba radhi kwa tukio lake hilo, na kuahidi kuchukua hatua ambazo zitahakikisha kosa hilo halitojitokeza tena
Utamadani wa kuwatumia wanawake warembo kwenye maonyesho ya bidhaa, umekuwa ni utaratibu wa wakawaida kwa makampuni ya elektroniki duniani. Ila tahadhari itumike, na kwa uangalifu wa karibu zaidi, aliongezea Bi susan Friedmann mtaalamu wa maswala ya ya biashara kwa kusema “ nilazima uzingatie unapofanya maonyesho kama haya, kinachoweza kukufunga Paducah yaweza kuwa sawa na Tokyo”

Kampuni ya Kidachi yaanzisha Makazi sayari ya Mars ifikapo mwaka 2023


Rover
Inaonekana kama ni nadharia ya kisayansi ambayo daima haiwezekani, kuwa halisi, kampunni ya Mars one ya Kidachi, imetamba kuwa wazo hilo ni halisia na mchakato mzima wa ujenzi wa makazi hayo utakamilika ifikapo mwaka 2023.
Kampuni hiyo binafsi inayo mpango madhubuti kilichobakia sasa ni Pesa ya kutosha kuufadhili huo mradi , vifaa na wana anga ambao wapo tayari kufanya safari ya moja kwa moja  kuelekea sayari ya mars pasi na kurudi kwenye sayari ya duniani. Ambapo na watategemewa kuishi huko kwa kipindi chote cha maisha yao
Mpangilio mzima ni kuanza kwa, kupeleka vifaa vya uchunguzi na usafirishaji(rovers), ambavyo vitakamilisha jukumu la kuteua eneo zuri  la ujenzi na kuanza kujenga makazi. Ifikapo mwaka 2022 kundi la kwanza litaelekea kwenye sayari hiyo, safari inayotegemewa kuchukua miezi saba, kuweka kambi katika makazi yao mapya.lengo likiwa ni kuanza maisha mapya na kuishi huko kwa kipindi chote cha maisha yao, kisha kila baada ya miaka miwili kundi jingine la watu litakuwa likienda kwenye makazi hayo.
Ikiwa inafananishwa na Big Brother, tayari mradi huo umepata baraka za kutosha kutoka kwa wadau wanaojihusisha na mambo ya anga kutoka nchi  mbali mbali duniani. Ambao watachangia vifaa vya ujenzi na kutoa mchango wa kitaalama pale itapohitajika. Ni mradi binafsi ambao hautegemeai pesa za walipa kodi kwa hiyo haitegemewi kutokea mifarakano yoyote au kusitishwa kwa  sababu za kisiasa au hila za wanasiasa.

Muazilishi wa mradi huo ndugu Bas Lansdorp, anatazamia kutumia mbinu ya kisasa. Ujenzi wa makazi hayo utakuwa ukirushwa hewani moja kwa moja na kutoa nafasi ya kila mmoja kuweza kuushuhudia ukiendelea.
Video ya Mars one imeshapata zaidi ya watazamaji 232, 000 tangu iliporushwa kwenye youtube,com
Tayari baadhi ya wanasayansi waliobobea wameanza kuonesha shaka juu ya mradi huo, kwamba upo kinadharia zaidi.
Kwa mujibu wa mtandao Mars one kuanzia mwakani wataanza uteuzi wa wana anga watakaoshiriki kwenye mradi huo

PROMETHEUS 3D IN CINEMAS

Tuesday, 5 June 2012

227


Google yaongeza upinzani kwa MICROSOFT kuinunua kampuni ya QUICKOFFICE



Kampuni ya google imekuwa ikiendeleza upinzani wake kwa kampuni ya microsoft kwa kitendo chake cha hivi karibuni kuinunua kampuni inayojishuhulisha na utengenezaji wa programu ya QUICKOFFICE,
Quickoffice ni programu inayofanya kazi kwenye simu,na komputa za mikononi lengo lake ikiwa ni kufungua mafaili yaliyo katika mfumo wa microsoft office.

Hii itaongeza upinzani kwa kampuni ya microsoft kwa kuviwezesha vifaa kama ipad na vingine ambavyo microsoft haija unda nakala ya programu ya microsoft office. kuweza kufanya kazi kwenye vifaa hivi na kuvipa uwezo wa  kufungua mafaili yaliyo katika mfumo huo.

Mkurugenzi wa kampuni ya microsoft amezikosoa programu zinazotengezwa na Google kwa kudai kuwa hazikidhi mahitaji ya watumiaji kwa ukamilifu.

Ingawa mapato ya kampuni ya quickoffice yanatokana na matangazo, programu hiyo imekuwa ikitumia na ikifanya kazi katika vifaa takribani milioni 400, ambapo kila programu inauzwa kati ya dola 15 hadi 20. na inawatoza wateja wake pesa kidogo kwa wale watakaohitaji programu hizo kuwa na uwezo wa ziada kama kuandika au kurekebisha.

Quikoffice yenye makao yake makuu nchini marekani katika jimbo la Texas linawafanyakazi 400 na ipo chini ya Alan Masarek ambaye aliianzisha kampuni hiyo miaka kumi iliopita,
Ambapo google yenye makao makuu yake nchini marekani pia, mwishoni mwa mwezi wa machi lilikuwa na jumla ya wafanyakazi 33 000, na ilijiongezea  wafanyakazi 20, 000 baada ya kukamilisha ununuzi wa kampuni ya Motorola Mobility kwa dola za kimarekani bilioni 12,5

China ya kopi na kupesti mji uliopo Austria



China umejenga mji kwa kuugerezea mji unaofanana na uliopo Austria. HUTZHOU ni kopi ya mji uitwao HALLSTATT uliopo nchini Austria, mradi huo umeghararimu takribani dolla za kimarekani milioni 940.
Hivi karibuni shirika la umoja wa taifa linalojihusisha na maswala ya elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO) liliutaja mji wa Hallstart kama moja ya miji inayovutia duniani( UNESCO WORLD HERITAGE).
China ikiwa kama nchi inayofahamika kwa kutengeneza vitu vya kunakiili, imekuja na kioja ambacho wengi hatuki kitegemea, na kiliwakwaza sana wakazi wa jiji la hallstart.
Mwanzoni serikali ya Austria ilipatwa na shaka juu ya uamuzi huo wa china, ila maelewano yalifanyika na wanategemea kushirikiana katika mambo mengine vile vile
Meya wa jiji la Hallstart alisafiri na jopo lake kutoka Austria hadi mjini HUTZHOU, na kuhudhuria ufunguzi, na kukukiri kuwa mwanzo wazo hilo la china lilizua utata.
Ni mategemeo ya wengi kwamba mji huo utakuwa kivutio kikubwa sana, takwimu zinaonyesha idadi ya wa china isiozidi 50 mwaka 2005 ilikuwa ikienda katika mji wa Hallstart iliongezeka  hadi kufikia maelfu hivi sasa liliesema jopo hilo la wadau kutoka Austria.
Ujenzi wa mji huo badi unaendelea, na upo chini ya mfabiashara mwenye mafanikio ya hali ya juu nchini humo.














Filamu ya “TheHunger Games” imejinyakulia tuzo nne...


Filamu ya “The Hunger Games” imejinyakulia tuzo nne za MTV za mwaka huu.


Bridesmaid, the punultimate Twilight installment na sehemu ya mwisho ya muendelezo wa filamu za Harry Potter  zilijipatia tuzo pia.


Russel Brand ndiye aliyeoongoza hafla hiyo , katika jiji la Universal, los Angeles
Jonny Depp alipata tuzo za heshima, MTV generation award.
 “ni sawa na kuondoka katika ulimwengu wa tuzo” sababu umeshafanya vitu vingi mno” alitania nyota huyo wa filamu za Pirates of the caribean.

Zawadi zingine zilienda kwa aliyekuwa nyota wa tamthilia ya Friends Jennifer Aniston, ambapo nafasi yake kama dakatari ma wa meno katika filanu “Horrible Bosses” ilimpatia wadhfa wa “best on screen”

“Harry potter and the Deathly Hallows pati 2” ilishinda tuzo ya filamu iliyokuwa na jopo bora na tuzo ya mashujaa (the best cast and best hero awards).  Wakati “Twilight saga Breaking Dawn pati 2” ilipata tuzo ya filamu ya mwaka.

Mundelezo wa filamu ya 

“Vampire” ilipata tuzo ya Busu 

bora, kwa miaka minne kwa mfululuizo.










Mwanadada Melisa McCarthy wa filamu ya "bridesmaid" alijinyakulia tuzo ya mchekeshaji bora.

Van Damme aongozana na Bintiye kwenye Tuzo za MTV

Van Damme na Bintiye Bianca


Maisha ya kimapenzi ya mwana sinema mashuhuri van Damme, yamekuwa ni yenye kupendeza miaka ya hivi karibuni, ikiwa amewahi kuoa mara tano, na kumuoa mmoja ya wake zake hao mara mbili. Kwa minajiri hiyo inakuwa vigumu kuotea ni nani ataye ambatana naye katika shuhuli kama hii kama mwenza wake katika tafrija kubwa kubwa kama hii.
Ila katika tuzo za MTV jumapili hii iliyopita aliambatana na Bintiye mwenye umri wa miaka 21.
Van Damme aliongozana na bintiye Bianca Bree (jina halisi: Bianca Van Varenberg, ambalo ni jina lake mwisho  Van Damme's ). Van damme ambaye ni nyota wa filamu ya expendables 2, alipozi na bintiye kwa ajili ya picha ya picha mbali mbli, huku kimwana  huyo akiwa amevalia kivazi kilichovutia hisia za wengi,
Bianca aliandika kwenye ukurasa wake wa twita kuhusiana na usiku huo “kama ambavyo sipendi kuuza sura, ila nilipata wakati mzuri sana” alifurahi mno kumuona Charlie sheen. Na akiendelea kumulezea nyota huyo wa filamu ya “ Anger Management” “ni  mwenye muonekano mzuri na ninampenda sana huyu jamaa kwa lolote lile”.
Bianca amekuwa akitokea katika filamu za baba yake tangu mwaka 2008, na kuna filamu tatu zinafata ikiwemo “ welcome to the jungle” ambaye yupo na kaka yake Kristopher Van Damme mwenye umri wa miaka 24. wote wakiwa ni watoto wa Van Damme na aliyekuwa mkewe mtunisha misuli Gladys Portugues waliofunga ndoa 1987-1992 na kuja kufunga ndoa tena mwaka 1999, ingawa Bianca anajaribu kufata njia yake binafsi tofauti na muelekeo wa familia yake.

Soda na Athari zake kwa Afya zetu


Meya wa jiji la new york Ndugu Michael Bloomberg ambaye ni mrithi wa aliyekuwa meya wa jiji hilo kabla yake Bi Hillary Clinton amelaumiwa kwa kitendo chake cha  kupendekeza soda zipigwe marufuku kwa kile kinachosemenaka kuwa zina mazara kiafya.pendekezo lake hilo limeonekana kuwa ni laki mabavu na lina pingana na sera ya "uhuru" ya nchini marekani. Je ni kweli soda ni hatari kwa afya yako?
Soda na tatizo la uzito wa mwili.
Karibia asilimia 66 ya wamarekani wanatatizo la kuwa na unene na uzito wa kupindukia.Ripoti iliotolewa na Chuo cha Afya ya JAmii cha Harvard nchini marekanai, imeonesha kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya unwaji na soda na ongezeko la uzito mwilini.Soda inachangia asimia saba ya wastani wa kalori zinazoingia miilini kwetu kwa kila siku.Kalori za kwenye soda zinaonekana nyepesi kulinganisha na kalori za kwenye chakula cha kawaida, kwa kuwa  chakula kitatufanya tushibe ila soda ni kimiminika, ambapo kalori zilizomo kwenye soda zitafyonzwa na kuingia katika mfumo wetu wa chakula pasi na kujisikia kushiba.Soda moja kwa siku yaweza changia ongezeko la hadi kilo 6.2 na mafuta mwilini kwa mwaka.
Soda na Magonjwa sugu
Soda ni sawa na dampo la sukari, iliyokatika mfumo wa fruktos.Kopo moja la soda ni sawa na vijiko vya chai  kumi vya sukari.Kitengo c ha Afya ya moyo marekani ili kuepusha madhara ya sukari kimeshauri mtu mzima kunywa chini ya vijiko sita vya sukari kwa siku, watoto visizidi vitatu, ila vijana walio wengi wanakunywa hadi vijiko 34 vya sukari kwa siku kutokana na kunywa vinywaji vitamu mara kwa mara.

Kubugia soda ya changia ongezeko la sukari kwenye damu, kwa kipindi fulani hii yaweza kuwa sababu ya maradhi kama kisukari, moyo, na pengine kansa.watafiti wakaendelea kusema asilimia 50 ya wanaotumia walau gramu 31 ya soda kila siku wana hatari ya kuugua maradhi ya dizaini hii, moja ya sababu inayoweza pelekea maradhi kwama stroku, kisukari na kusinyaa kwa mishipa ya damu.
Hii inaashiria ongezeko la unywaji wa soda kwa watu wazima itapelekea ongezeko la maradhaki haya katika miongo ijayo.
Soda na afya ya mifupa.
Tatizo jingine kwa vijana ni tatizo la afya ya mifupa, kama ilivyozoeleka kwa vijana na hasa watoto kupenda kunywa soda na vinywaji vitamu kwa wingi, na kunywa maziwa kwa uchache
Maziwa yana madini ya calcium, madini muhimu katika ukomavu wa mifupa, kama ilivyo kwa protini na virutubisho vingine vilivyomo kwenye maziwa.soda ina madini ya fosfeti., madini ambayo yanaweza athiri ujazo wa mifupa.  Iwapo itaingia mwilini kwa wingi kulinganisha na kiwango cha calcium. Tafiti zimethitisha kuna uhusiano wa karibu baina ya unywaji wa soda na tatizo la mifupa kwa wanawake watu wa wazima.
Soda na Kuoza kwa meno
Umakini umeelekezwa sana kwenye uhusiano wa soda na ongezeko la uzito mwilini. Uhusiano wa soda na athari zake kwa meno halijatazamiwa kwa kutosha.athari iliyopo haitokani tuu na sukari iliopo kwenye soda, bali hata kemikali zilizomo kwenye vinywaji vitamu, vya weza changia uharibifu wa meno kwa fujo.
Ni juu yetu kupima uzito wa maelezo haya katika kuamua kwamba soda inafaida kwetu au laa, ingawa zipo soda ambazo hazina sukari, Diebetic soda. Changamoto inabakia kwa serikali yetu na sisi wenyewe

Monday, 4 June 2012

WASIFU WA KOCHA DI MATTEO


Roberto Di Matteo, amezaliwa 29 Mei 1970. Ni mwanasoka wa zamani kutoka nchini Itali na ndiye kocha wa mpito wa timu ya Chelsea kwa msimu ulioishia mwaka 2012. Kipindi anacheza soka, alicheza kama kiungo katika klabu ya Uswiss Schaffhausen, Zurich na Aarau kabla ya kujiunga na klabu ya Lazio na Chelsea ya Uingereza. Aliichezea timu ya Italy mara 34, akifunga jumla ya magoli mawili, alicheza kwenye kombe la Euro mwaka 1996 na Kombe la dunia 1998.
Alistaafu kama mchezaji Februari 2002 akiwa na umri wa miaka 31, baada ya kuandamwa na matatizo ya majeruhi. Tangu hapo amekuwa akiziongoza kama kocha timu, Milton Keynes Dons, West Bromwich Albion na Chelsea. Akiwa kama kocha wa Chelsea amefanikiwa kushinda kombe la FA 2012 na kombe la klabu bingwa UEFA, ikiwa ndio ushindi wa mara ya kwanza kwa timu hiyo ya Chelsea.

Switzerland na Lazio
Amezaliwa Uswis, Wazazi wake ni raia wa Itali kutoka mji wa Paglieta, Abruzzo, Di Matteo alinza safari yake ya soka kwa kuichezea klabu ya Uswis Schaffhausen, kabla ya kujiunga na klabu ya Aarau mwaka 1991. Alitwaa ubwinga wa Nationalliga A, akiwa na klabu ya Aaru mwaka 1993.Ligi hiyo ikiwa ni ligi ya 14 kwa ubora barani Ulaya kwa mujibu wa UEFA. Katika kipindi hicho hicho alifanikiwa kujinyakulia tuzo ya uchezaji bora wa mwaka, Mwaka 1993 alisaini uhamisho bure  kipindi cha majira ya joto na kuelekea kuelekea klabu ya Lazio. Di Matteo alitokea kuchezea timu ya Lazio mara kwa mara na ndipo alipoanza kutokea  kwenye kikosi cha Timu yake ya Taifa ya Itali kipindi anachezea klabu yake ya jijini Roma.
Hata hivyo mfarakano baina yake na kocha wake ZdenÄ›k Zeman, baada ya kosa la kiulinzi lililopelekea kufungwa na timu ya Internazionale, ulimaliza safari yake na timu ya Lazio, matokeo yake akasainiwa na Ruud Gullit wa Klabu ya Uingereza kwa dau lilioweka rekodi ya £ 4.9 milioni.

Chelsea
Di Matteo alifunga goli la ushindi dhidi ya Middlesbrough katika mchezo wa nyumbani akiwa na klabu yake ya Chelsea katika mchezo wake wa kwanza.Uwezo wake wa kutoa pasi zenye uwezo wa hali ya juu na mashuti ya mbali yenye usahihi, ulimfanya awe ni mmoja wa wachezaji wenye uwezo na msukumo wa hali ya juu wa klabu yake ya Chelsea mwishoni mwa miaka ya tisini. Alichangia magoli tisa. Ikiwemo misaada ya umbali mrefu dhidi ya Tottenham Hotspur na Wimbledon. Aliisaidia Klabu yake kumaliza ligi ikiwa ya sita katika msimamo wa ligi, ikipata mafanikio ya hali ya juu tangu msimu wa mwaka 1989-1990, nakufanikiwa kufika katika fainali la kombe la FA mwaka 1997 Wembley. Mara tu baada mchezo huo kuanza ndani ya sekunde 42 alifunga goli dhidi ya Middlesbrough, Di Matteo alifunga goli la ufunguzi umbali wa yadi 30 na Chelsea kushinda 2-0.goli la Dimatteo ndio lilikuwa goli lililowahi kufungwa mapema zaidi hadi rekodi hiyo ilipovunjwa mwaka 2009 na Louis Saha wa Everton.
Msimu uliofata Di Matteo aliendelea kudhihirisha thamani yake kwa timu yake, kwa kupachika magoli kumi na kutoa  misaada ya hapa na pale, na Chelsea kuelekea kudai Footbal League Cup and na Winners Cup. Na kujipatia heshima ya Baralni  ulaya kwa mara nyingine tangu mwaka 1971 kwa kushinda dhidi ya Middlesbrough, Di M\tteo alifunga goli la pili, Di Matteo alicheza kati kama kiungo akiwa pembeni ya Gustavo Povet, Dennis Wise na Dan patrescu katika msimu wa mwaka 1998-99 ambapo Chelsea ilimaliza wa tatu

Katika msimu wa mwaka 1999-2000 Di Matteo alitolewa kikosini kutokana na majeraha ila aliridu mwishoni mwa msimu na kufunga magoli muhimu, likiwemo goli lake la tatu la ushindi ndani ya Wembley kwa mara nyingine katika kombe la FA, katika mchezo mgumu Di Matteo alitumia nafasi vizuri iliotokana na kosa lililofanywa na kipa wa Aston Villa David James katika dakika ya 71 na kujipatia goli la ushindi, na kuwazawadia Chelsea kwa mara nne katika kipindi cha miaka mitatu. Hii ilimfanya Di Matteo Aseme” ni aibu kuona wanauteketeza , umekuwa ni uwanja wenye bahati sana kwangu”

Mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2000 na 2001, alijikuta akivunjika mguu mara tatu katika kombe la UEFA dhidi ya St gallen klabu ya Uswisi na kutocheza kwa miezi 18 iliofata. Februari 2002 alitupilia mbali matumaini ya kurudi kucheza akitoka kwenye majeruhi aliyoyapata na kustaafu katika umri wa miaka 31.
“kama shukrani ya mchango kutoka kwa kiungo uliochangia mabadiliko ya klabu” kocha wa kipindi hicho Claudio Ranieri alimpa heshima ya kukiongoza kikosi cha Chelsea  katika fainali za kombe la FA 2002, ambapo ilipoteza dhidi ya Arsenal kwa 2-0.
Di Matteo alichaguliwa kama mchezaji wa Kihistoria wa klabu ya Chelsea. Katika miaka sita alipokuwa Chelsea aliichezea Chelsea mara 175 nakushinda magoli 26, hakuwahi  kupoteza uwanjani Old Trafford

Kimataifa

Di Matteo alitokea katika kikosi cha timu ya Itali kwa mara ya kwanza 16 Novemba 1994 ndani ya uwanja wa Stadio La Favorita, Palermo, Sicily. Aliingia uwanjani dakika ya 55 kama mbadala wa Demetro Albertinias, Itali ilipoteza 2-1 dhidi ya Croatia katika mechi za kufuzu Euro 1996.Alianza mwanzoni mwa mchezo katika mchezo wake wa pili katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Uturuki tarehe 21 Desemba 1994 katika uwanja wa Stadio Adriatico ndani Pescara. Ambapo ilishinda 3-1. Aliendelea kucheza timu yake ya Itali katika ngazi ya makundi 1996 dhidi ya Urusi na Ujerumani

Goli lake la kwanza alifunga kwenye mchezo wake wa 23 akiwa na timu yake ya taifa, katika michezo ya kufuzu kombe la Dunia la mwaka 1998 mnamo 30 April 1997, Itali ilishinda 3-0 dhidi ya Poland.Di matteo.DI Matteo alifunga goli moja la ziada, dhidi ya Slovakia Januari 1998. Alikuwemo kwenye kikosi cha kombe la dunia la mwaka 1998 na kuchezea michezo miwili ya ngazi ya makundi dhidi ya Chile na Cameroon. Mechi dhidi ya Cameroon Montpeller ndiyo uliokuwa mchezo wake wa mwisho kuichezea timu yake ya Itali.

Akiwa kama Kocha wa Chelsea

Baada ya kushindwa kufanikiwa kuwa meneja wa timu ya Birmingham City. Di Matteo aliteuliwa kuwa kocha msaidizi wa André Villas-Boas (kocha mpya wa Chelsea 29 Juni 2011).
Baada ya kufukuzwa kazi kocha André Villas-Boas, Di Matteo alipewa madaraka ya mpito na kuiongoza timu ya Chelsea kuanzia March 2012.Aliendelea kutambulika kama kocha wa mpito kwa mujibu wa klabu ya Chelsea. Alianza kupata mafanikio ya moja kwa moja mara tuu baada ya kupewa timu, alishinda dhidi ya Birmingham City, katika mzunguko wa tano wa kombe la FA, Stoke city katika ligi ya Uingereza na Napoli katika mzunguko wa 16 kombe la Klabu bingwa UEFA nakushinda 4-1 baada ya mechi ya kwanza Chelsea kupoteza 3-1, walipokuwa chini ya uongozi wa André Villas-Boas
Di Matteo alishinda dhidi ya Tottenham kwenye nusu fainali za kombe la FA na Dhidi ya Benfica kwenye robo fainali ya UEFA, tarehe 24 April  aliipatishia Chelsea ushindi dhidi ya Barceloma kwenye nusufainali kwa jumla ushindi wa 3-2 nyumbani na  ugenini, na kuwa toa barcelona waliokuwa wakitetea ubingwa wa klabu bingwa UEFA, Mei 5 Chelsea ilishinda dhidi ya Liverpool 2-1 kwenye mchezo wa fainali wa kombe la FA ndani ya uwanja wa wembley.

19 Mei Di Matteo aliingoza Chelsea nakushindaUEFA kwa kuishinda klabu ya Ujerumani Bayern Munich, ushindi mnono ulipatikana kwa penati, na kuifanya Chelsea kushinda kombe la UEFA kwa mara ya kwanza na kuifanya ifuzu katika msimu wa klabu bingwa ulaya wa 2012-2013, baada ya kuto maliza miongoni mwa timu nne ambazo zingesonga mbele, hii ikapelekea pelekea kutolewa kwa wapinzani wao wa jijini  London Tottenham Hotspur kutofuzu katika kinyanganyoro hicho cha UEFA.
Maisha yake ya Kifamilia
Di Matteo ameo na ana watoto wa tatu, na kwa sasa hv anaishi Leamington Spa, Warwickshire



Wanamichezo Mashuhuri wanaolipwa zaidi Ulimwenguni


Wanamichezo mashuhuri wenye mvuto wa kibiashara zaidi duniani, ambao wamekuwa miongoni mwa orodha ya watu 100 mashuhuri duniani, orodha yao imesambaa kutoka kwenye  michezo tofauti tofauti duniani.wanamichezo 17 wamefuzu kuwemo katika orodha ya watu mashuhuri 100( wanaume wakiwa 14 na wanawake 3) wote hawa wakitokea katika michezo saba tofauti na wamezaliwa katika nchi 9 tofauti tofauti.

Akiungoza msafara huu ni Tiger woods, ambaye ni wa 12 kutoka wa 6 kwa mwaka 2011.Mapato ya Tiger woods yameporomoka kutoka dola milioni 75 kwa mwaka jana hadi dola milioni 58 kwa mwaka huu, ikichangiwa na kujiondoa kwa wadhamini wake wakubwa kama Gillete, ila bado ameendelea kushikilia kiwango cha juu cha kulipwa kama mwanamichezo duniani, uwiano wa umaarufu wake umewazidi wanamichezo, wote jina lake likitajwa sana kwenye vyombo vya habari hasa runinga na redio, akiwa wa sita miongoni kwa watu mashuhuri 100 kwa ujumla.

Wanasoka waongoza miongoni kwa wanamichezo wa kiume, ikiwa ni  mchezo pekee wenye wanamichezo watatu wakiume wakitokea katika aina moja ya mchezo, ni David Beckham(32), Christiano Ronaldo( 44) na Lionel Messi(50).Ukiachilia mbali  kiwango kikubwa cha mapato yao, wote watatu wamekuwa na wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii,  wote kwa ujumla wakiwa na wafuasi facebook milioni 95. Kitendo hicho kimekuwa kikiwaongezea thamani hasa kimatangazo kwa wadhamini kama Nike(Ronaldo) na Adidas(beckham, Messi)


LI Na
Wanamichezo wakike watatu miongoni mwa watu mashuhuri 100 duniani wametokea katika aina moja ya mchezo , Maria sharapova kwa mara nyingine akiongoza kutoka dola millioni 24.6 hadi dola milioni 26 kwa kipindi cha miezi 12 iliopita, ambapo Serena Williams(76) akiwa na mvuto wa aina yake katika medani ya tennis, na hatimaye mwanatenis Li Na(88) kutoka china ni mgeni katika dira hili, mwaka jana kwenye Grand Slam akishinda taji la French Open.Aliendeleza mafanikio nje ya viwanja vya tennis akijipatia mikataba minono iliompa dola za kimarejani milioni 7 kutoka Mercedes na Samsung baada ya ushindi wake huo wa Jijini paris. Watu mashuhuri wageni wenza wa Li Na ni pamoja na Rihanna na Kim Kardashian

Wana NBA wameporomoka kwa namna Fulani kutokana na kuwa nje kimechezo kwa muda wa miezi mitano, ikiwagharamu asilimia 20 ya mapato yao,  ambapo msimu ulifupishwa hadi kuwa na michezo 66 kwa kila timu. Matokeo haya yamewapeleka Dwayne Wade na Dwight Howard kutoka kuwepo katika orodha ya mwaka huu, wakiungana na wenzao Charlie sheen na Jay leno



Kufanikisha kuwepo katika orodha ya watu mashuhuri 100 miongoni mwa wanamichezo inahitaji umaarufu wa hali ya juu na Mkwanja Mnene.Mwana Michezo bora wa Super Bowl kwa kipindi cha misimu mitatu Bingwa Tom Brady ndiye mwenye mapato madogo zaidi kulinganisha na wenzake katika msimu wa miezi 12 ilipiopita miongoni mwa wanaume kwa kujipatia dola milioni 27.
Je ni wanamichezo gani wanaotegemewa kuwemo katika orodha ijayo? Ni mwana kikapu Kevin Durant ambaye amekuwa akiongoza kwa mfululizo katika ufungaji kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo pamoja na |Derrick Roses ambaye ongezo la mkataba wake kwa Timu yake ya Chicago Bulls(milioni $95 kwa kipind cha miaka 5) na Adidas(milioni $ 185 kwa zaidi ya miaka 13)




Sunday, 3 June 2012

The Most Powerful Athletes


A MAY 2012 ARTICLE ( )
The world’s most powerful celebrity athletes span across sports and the globe. The 17 athletes that qualified for our 2012 Celebrity 100 (14 men and 3 women) play seven different sports and were born in nine different countries.
Leading the way among athletes isTiger Woods, who ranks No. 12 overall–down from No. 6 in 2011. Woods’s annual income dropped to $58 million from $75 million due to continued sponsor defections like Tag Heuer and Gillette, but he remains one of the highest paid athletes in the world. His fame quotient exceeds any other athlete as mentions of his name on TV and the radio were tops among athletes and sixth highest among all celebrities.
Soccer players rule among the men, as the only sport where three players made the cut with David Beckham (No. 32), Cristiano Ronaldo (No. 44) andLionel Messi (No. 50). In addition to their prodigious incomes, all three are social media giants with a combined 95 million Facebook followers. The avid following makes them more attractive and valuable to sponsors like Nike(Ronaldo) and Adidas (Beckham, Messi).
The three female athletes are from the world of tennis (Nascar’s Danica Patrick just missed cut). Maria Sharapova (No. 71) remains the world’s highest paid female athlete with earnings of $26 million over the past 12-months, while Serena Williams (No. 76) is the most compelling figure in women’s tennis. Li Na (No. 88) is a newcomer who last year became the first Chinese player to win a Grand Slam event with her French Open title. She scored big off the court with seven multimillion-dollar endorsement deals including Mercedes and Samsung after her Paris triumph. Li’s fellow newcomers include Rihanna and Kim Kardashian.
NBA players got dinged by the five-month NBA lockout, which cost players 20% of their paychecks when the season was reduced to 66 game per team. The reduced incomes cost All-Stars Dwyane Wade and Dwight Howard their spots after appearing on the Celebrity 100 in 2011. They join other notable drop-offs like Charlie Sheen and Jay Leno.
Making the final cut for the Celebrity 100 among sports stars requires a massive level of fame and a thick wallet. Three-time Super Bowl champ Tom Brady had the lowest earnings over the past 12-months, among the men, at $27 million. The cut-off among the women was $13 million, which Serena Williams earned over the past year.
What athletes are destined to make future Forbes Celebrity lists? We identified two NBAers that are included among our rising stars. Kevin Durant won his third straight NBA scoring crown during this season and has established himself as one of the NBA’s best players in his first five seasons in the league. Nike snapped up Durant in 2007 with a seven-year, $60 million deal. Derrick Rose’s income is set to explode next season when contract extensions with the Chicago Bulls ($95 million over five years) and Adidas ($185 million over 13 years) kick in.
-

PAPA WEMBA -- MARIA VALENCI

Wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani Tiger Woods na Kobe Bryant.


Toleo la mwaka 2011 May 31

Mafanikio ya mwanamichezo Tiger Woods, imekuwa ikidorora kwa kipindi cha miaka miwili iliopita. Wadhamini wakubwa kama Accenture, AT&T, Gillette na PepsiCo wamejitoa katika udhamini. Tangu November mwaka jana,pindi tu tukio la ajali ya gari lilipojitokeza na muendelezo wa kashfa zilizofata.

Biashara yake ya kudizain viwanja vya golf nayo iliporomoka kifaida kutoka na mporomoko wa hali ya uchumi duniani.Na nuksi ya muendelezo wa kutoshinda kwenye vinyanganyiro vya mashindano ya golf  kwa kipindi cha miezi 20 na ushee, imepelekea gwiji huyo aliyekuwa mwanamichezo namba moja katika michezo ya golf kuwa wa 13 duniani, na mapato yake ya kipungua kwa dola milioni 50, kwa kipindi cha miaka 2 miwili iliyopita.

Pamoja na yote hayo Tiger Woods bado ndiye mwanamichezo namba moja ulimwenguni kwa kulipwa pesa nyingi, na hakuna anayemkaribia kwa karibu, Akipata dola za kimarekani milioni 75 kwa kipindi cha miezi 12 iliopita, akimuacha kwa mbali sana Kobe Bryant aliyejitengezea dola milioni 53 za kimarekani katika msimu huo huo.

Mafanikio yake kwa zaidi ya asilimia hamsini yametokana na wadau wake wa muda mrefu Kampuni ya Nike na Electronic Arts, ambao wote hawa waliingia naye mkataba kuanzia mnamo mwaka 1998 akipokuwa rasmi mwanamichezo professional,

Kwa mara nyingine tena wanamichezo wa kike, wakiwa nyuma katika takwimu hizi za wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani.Mcheza Tennis Mara Sharapova ndiye mwanamke pekee aliyeweza kupenya katika orodha ya wanamichezo 50 wanaolipwa zaidi duniani, ni wa 29 akijipatia dola milioni 24.2, kwa kiasi kikubwa kutoka kwa wadau wake kama Nike.


HABARI HII NI TOLEO LA MWAKA JANA TAREHE 31 MAY 2011, KWA MUJIBU WA TAKWIMU ZA FORBES


Friday, 1 June 2012

Chagas: Is tropical disease really the new AIDS?


Chagas: Is tropical disease really the new AIDS?

Chagas, a tropical disease spread by insects, is causing some fresh concern following an editorial—published earlier this week in a medical journal—that called it "the new AIDS of the Americas."
More than 8 million people have been infected by Chagas, most of them in Latin and Central America. But more than 300,000 live in the United States.
The editorial, published by the Public Library of Science's Neglected Tropical Diseases, said the spread of the disease is reminiscent of the early years of HIV.
"There are a number of striking similarities between people living with Chagas disease and people living with HIV/AIDS," the authors wrote, "particularly for those with HIV/AIDS who contracted the disease in the first two decades of the HIV/AIDS epidemic."
Both diseases disproportionately affect people living in poverty, both are chronic conditions requiring prolonged, expensive treatment, and as with patients in the first two decades of the HIV/AIDS epidemic, "most patients with Chagas disease do not have access to health care facilities."
Unlike HIV, Chagas is not a sexually-transmitted disease: it's "caused by parasites transmitted to humans by blood-sucking insects," as the New York Times put it.
"It likes to bite you on the face," CNN reported. "It's called the kissing bug. When it ingests your blood, it excretes the parasite at the same time. When you wake up and scratch the itch, the parasite moves into the wound and you're infected."
"Gaaah," Cassie Murdoch wrote on Jezebel.com, summing up the sentiment of everyone who read the journal's report.
Chagas, also known as American trypanosomiasis, kills about 20,000 people per year, the journal said.
And while just 20 percent of those infected with Chagas develop a life-threatening form of the disease, Chagas is "hard or impossible to cure," the Times reports:
The disease can be transmitted from mother to child or by blood transfusion. About a quarter of its victims eventually will develop enlarged hearts or intestines, which can fail or burst, causing sudden death. Treatment involves harsh drugs taken for up to three months and works only if the disease is caught early.
"The problem is once the heart symptoms start, which is the most dreaded complication—the Chagas cardiomyopathy—the medicines no longer work very well," Dr. Peter Hotez, a researcher at Baylor College of Medicine and one of the editorial's authors, told CNN. "Problem No. 2: the medicines are extremely toxic."
And 11 percent of pregnant women in Latin America are infected with Chagas, the journal said.