sikika
Wednesday, 6 June 2012
Picha kwa Hisani ya National Geographic Channel
Mabilionea Vijana Duniani
Mabilionea wanne vijana wanahusika moja
kwa moja na facebook, wawili ni watoto wa aliyekuwa Waziri mkuu wa Lebanon
Hayati Rafic Hariri, na mmoja ni mwananke. Wafuatao ni mabilionea vijana
kwa mujibu wa mtandao wa peekyou.com
1. Mark Zuckerberg
Mark Zuckerberg ambaye sasa anaumri wa
miaka 28, alizindua facebook kwenye bweni lake kipindi
anasoma chuo na amekuwa huku akizungukwa na wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa
duniani. Utajiri umeongezeka kwa kasi baada ya kuiorodhesha facebook
kwenye soko la hisa, anathamani ya dola bilioni 15 kwa mujibu wa takwimu. Ndiye anaengoza
katika orodha ya mabilionea vijana.
2. Scott Duncan
Sasa akikaribia umri wa umri wa miaka 30, amejipatia utajri
wake kwa kuridhi mali
kutoka kwa marehemu mzee wake, ambaye alianzisha kampuni ya Energy. Anasadikika
kuwa na thamani ya dola bilioni 4 za kimarekani
Moskovitz alifahamina na Mark tangu wapo chuoni, alifanya kazi Facebook kipindi cha awali cha ukuaji wa kampuni ya facebook, Hivi karibuni ameamua
kujihusisha na michakato mingine ikiwemo na shuhuli za misaada, kwa mujibu wa
forbes anathamani ya dola bilioni 3.5
4.Sean Parker
Muanzilishi wa Kampuni ya Napster na
raisi wa kwanza wa Facebook anathamani ya zaidi dola bilioni mbili. Parker mwenye
umri wa miaka 32, amekuwa mshauri mkuu wa zuckerberg na ndiye anayefahamika
zaidi kwa kumshauri Mark kubadilisha jina la kampuni ya facebook kutoka kwenye
kuitwa “ the facebook” hadi “facebook”. Na ndiye aliyekuwa miongoni mwa watu wa
mwanzo kuwekeza kwenye mtandao wa muziki wa Spotify
5. Eduardo Saverin
Ni mwanzilishi mwenza wa facebook
ambaye sasa anamakadirio wa utajiri wenye thamani ya dola bilioni 2, ila
ilimlazimu kupigania hadhi yake hiyo, aliishitaki kampuni ya
facebook, yalifanyika maelewano nje ya mahakama. Kama
ilivyo wasilishwa kwenye filamu ya "The social Network", Saverin mwenye umri wa
miaka 30, amekulia kwenye familia ya kitajiri anafahamika kama mpenda kula bata.
Wengineo ni
pamoja na ...
Fahdi Hariri
Robert Pera
Ayman Hariri
Yang Huiyan
Albert Von Thurn Und
Taxis
Tweet kutoka kampuni ya Asus iliozua Utata
Ni ujumbe
wa twita, uliozua mijadala kwenye mitandao ya intaneti kwa kushutumiwa kuwa
unamdhalilisha mwanamke. Kampuni ya Electronics Asus iliufuta ujumbe wake huo ulioambatanishwa
na picha inayomuonyesha mwanamke akielezea bidhaa mpya ya kampuni hiyo mara tu
baada malalamiko kuanza.
Ni
picha iliopigwa kwa kuuchukua upande wa nyuma ya mwili wa mrembo huyo ikiambatana
na ujumbe unaosema “ picha ya nyuma ni nzuri sana ,
kama
ilivyo Transformer AIO”
Posti hiyo ilipotea
kwa haraka sana, ila walichelewa kwani ilishadakwa na watu kuanza kuichangia na
wenzao, na kusambaa kwa kasi kwenye mitandao mingine na malalamiko na shutuma kuanza kuelekezwa kwa
kampuni hiyo.hata hivyo kampuni ya Asus iliomba radhi kwa tukio lake hilo, na
kuahidi kuchukua hatua ambazo zitahakikisha kosa hilo halitojitokeza tena
Utamadani
wa kuwatumia wanawake warembo kwenye maonyesho ya bidhaa, umekuwa ni utaratibu
wa wakawaida kwa makampuni ya elektroniki duniani. Ila tahadhari itumike, na
kwa uangalifu wa karibu zaidi, aliongezea Bi susan Friedmann mtaalamu wa
maswala ya ya biashara kwa kusema “ nilazima uzingatie unapofanya maonyesho
kama haya, kinachoweza kukufunga Paducah yaweza kuwa sawa na Tokyo”
Kampuni ya Kidachi yaanzisha Makazi sayari ya Mars ifikapo mwaka 2023
![]() |
| Rover |
Kampuni hiyo binafsi inayo mpango madhubuti kilichobakia sasa ni Pesa
ya kutosha kuufadhili huo mradi , vifaa na wana anga ambao wapo tayari kufanya
safari ya moja kwa moja kuelekea sayari
ya mars pasi na kurudi kwenye sayari ya duniani. Ambapo na watategemewa kuishi huko kwa kipindi chote cha maisha yao
Mpangilio mzima ni kuanza kwa, kupeleka vifaa vya uchunguzi na usafirishaji(rovers),
ambavyo vitakamilisha jukumu la kuteua eneo zuri la ujenzi na kuanza kujenga makazi. Ifikapo
mwaka 2022 kundi la kwanza litaelekea kwenye sayari hiyo, safari inayotegemewa
kuchukua miezi saba, kuweka kambi katika makazi yao
mapya.lengo likiwa ni kuanza maisha mapya na kuishi huko kwa kipindi chote cha
maisha yao ,
kisha kila baada ya miaka miwili kundi jingine la watu litakuwa likienda kwenye
makazi hayo.
Ikiwa inafananishwa na Big Brother, tayari mradi
huo umepata baraka za kutosha kutoka kwa wadau wanaojihusisha na mambo ya anga
kutoka nchi mbali mbali duniani. Ambao
watachangia vifaa vya ujenzi na kutoa mchango wa kitaalama pale itapohitajika.
Ni mradi binafsi ambao hautegemeai pesa za walipa kodi kwa hiyo haitegemewi kutokea
mifarakano yoyote au kusitishwa kwa
sababu za kisiasa au hila za wanasiasa.
Muazilishi wa mradi huo ndugu Bas Lansdorp,
anatazamia kutumia mbinu ya kisasa. Ujenzi wa makazi hayo utakuwa ukirushwa
hewani moja kwa moja na kutoa nafasi ya kila mmoja kuweza kuushuhudia
ukiendelea.
Video ya Mars one imeshapata zaidi ya watazamaji 232, 000 tangu iliporushwa
kwenye youtube,com
Tayari baadhi ya wanasayansi waliobobea wameanza kuonesha
shaka juu ya mradi huo, kwamba upo kinadharia zaidi.
Kwa mujibu wa mtandao Mars one kuanzia mwakani
wataanza uteuzi wa wana anga watakaoshiriki kwenye mradi huo
Subscribe to:
Posts (Atom)








