Tuesday, 5 June 2012

Google yaongeza upinzani kwa MICROSOFT kuinunua kampuni ya QUICKOFFICE



Kampuni ya google imekuwa ikiendeleza upinzani wake kwa kampuni ya microsoft kwa kitendo chake cha hivi karibuni kuinunua kampuni inayojishuhulisha na utengenezaji wa programu ya QUICKOFFICE,
Quickoffice ni programu inayofanya kazi kwenye simu,na komputa za mikononi lengo lake ikiwa ni kufungua mafaili yaliyo katika mfumo wa microsoft office.

Hii itaongeza upinzani kwa kampuni ya microsoft kwa kuviwezesha vifaa kama ipad na vingine ambavyo microsoft haija unda nakala ya programu ya microsoft office. kuweza kufanya kazi kwenye vifaa hivi na kuvipa uwezo wa  kufungua mafaili yaliyo katika mfumo huo.

Mkurugenzi wa kampuni ya microsoft amezikosoa programu zinazotengezwa na Google kwa kudai kuwa hazikidhi mahitaji ya watumiaji kwa ukamilifu.

Ingawa mapato ya kampuni ya quickoffice yanatokana na matangazo, programu hiyo imekuwa ikitumia na ikifanya kazi katika vifaa takribani milioni 400, ambapo kila programu inauzwa kati ya dola 15 hadi 20. na inawatoza wateja wake pesa kidogo kwa wale watakaohitaji programu hizo kuwa na uwezo wa ziada kama kuandika au kurekebisha.

Quikoffice yenye makao yake makuu nchini marekani katika jimbo la Texas linawafanyakazi 400 na ipo chini ya Alan Masarek ambaye aliianzisha kampuni hiyo miaka kumi iliopita,
Ambapo google yenye makao makuu yake nchini marekani pia, mwishoni mwa mwezi wa machi lilikuwa na jumla ya wafanyakazi 33 000, na ilijiongezea  wafanyakazi 20, 000 baada ya kukamilisha ununuzi wa kampuni ya Motorola Mobility kwa dola za kimarekani bilioni 12,5

No comments:

Post a Comment