Wanamichezo
mashuhuri wenye mvuto wa kibiashara zaidi duniani, ambao wamekuwa miongoni mwa orodha ya watu 100 mashuhuri duniani, orodha yao imesambaa kutoka kwenye michezo tofauti tofauti duniani.wanamichezo 17
wamefuzu kuwemo katika orodha ya watu mashuhuri 100( wanaume wakiwa 14 na
wanawake 3) wote hawa wakitokea katika michezo saba tofauti na wamezaliwa
katika nchi 9 tofauti tofauti.
Akiungoza
msafara huu ni Tiger woods, ambaye ni wa 12 kutoka wa 6 kwa mwaka 2011.Mapato
ya Tiger woods yameporomoka kutoka dola milioni 75 kwa mwaka jana hadi dola
milioni 58 kwa mwaka huu, ikichangiwa na kujiondoa kwa wadhamini wake wakubwa kama Gillete,
ila bado ameendelea kushikilia kiwango cha juu cha kulipwa kama mwanamichezo
duniani, uwiano wa umaarufu wake umewazidi wanamichezo, wote jina lake likitajwa sana kwenye vyombo
vya habari hasa runinga na redio, akiwa wa sita miongoni kwa watu mashuhuri 100 kwa
ujumla.
Wanasoka
waongoza miongoni kwa wanamichezo wa kiume, ikiwa ni mchezo pekee wenye wanamichezo watatu wakiume wakitokea katika aina moja ya mchezo, ni David Beckham(32), Christiano Ronaldo(
44) na Lionel Messi(50).Ukiachilia mbali
kiwango kikubwa cha mapato yao, wote watatu wamekuwa na wafuasi wengi
katika mitandao ya kijamii, wote kwa ujumla wakiwa na wafuasi facebook milioni
95. Kitendo hicho kimekuwa kikiwaongezea thamani hasa kimatangazo kwa wadhamini
kama Nike(Ronaldo) na Adidas(beckham, Messi)
![]() |
| LI Na |
Wana
NBA wameporomoka kwa namna Fulani kutokana na kuwa nje kimechezo kwa muda wa
miezi mitano, ikiwagharamu asilimia 20 ya mapato yao , ambapo msimu ulifupishwa hadi kuwa na michezo
66 kwa kila timu. Matokeo haya yamewapeleka Dwayne Wade na Dwight Howard kutoka
kuwepo katika orodha ya mwaka huu, wakiungana na wenzao Charlie sheen na Jay
leno
Kufanikisha
kuwepo katika orodha ya watu mashuhuri 100 miongoni mwa wanamichezo inahitaji
umaarufu wa hali ya juu na Mkwanja Mnene.Mwana Michezo bora wa Super Bowl kwa
kipindi cha misimu mitatu Bingwa Tom Brady ndiye mwenye mapato madogo zaidi kulinganisha
na wenzake katika msimu wa miezi 12 ilipiopita miongoni mwa wanaume kwa
kujipatia dola milioni 27.
Je ni
wanamichezo gani wanaotegemewa kuwemo katika orodha ijayo? Ni mwana kikapu Kevin
Durant ambaye amekuwa akiongoza kwa mfululizo katika ufungaji kwa kipindi cha
miaka mitatu mfululizo pamoja na |Derrick Roses ambaye ongezo la mkataba wake
kwa Timu yake ya Chicago Bulls(milioni $95 kwa kipind cha miaka 5) na Adidas(milioni
$ 185 kwa zaidi ya miaka 13)



No comments:
Post a Comment