Wednesday, 6 June 2012

Kampuni ya Kidachi yaanzisha Makazi sayari ya Mars ifikapo mwaka 2023


Rover
Inaonekana kama ni nadharia ya kisayansi ambayo daima haiwezekani, kuwa halisi, kampunni ya Mars one ya Kidachi, imetamba kuwa wazo hilo ni halisia na mchakato mzima wa ujenzi wa makazi hayo utakamilika ifikapo mwaka 2023.
Kampuni hiyo binafsi inayo mpango madhubuti kilichobakia sasa ni Pesa ya kutosha kuufadhili huo mradi , vifaa na wana anga ambao wapo tayari kufanya safari ya moja kwa moja  kuelekea sayari ya mars pasi na kurudi kwenye sayari ya duniani. Ambapo na watategemewa kuishi huko kwa kipindi chote cha maisha yao
Mpangilio mzima ni kuanza kwa, kupeleka vifaa vya uchunguzi na usafirishaji(rovers), ambavyo vitakamilisha jukumu la kuteua eneo zuri  la ujenzi na kuanza kujenga makazi. Ifikapo mwaka 2022 kundi la kwanza litaelekea kwenye sayari hiyo, safari inayotegemewa kuchukua miezi saba, kuweka kambi katika makazi yao mapya.lengo likiwa ni kuanza maisha mapya na kuishi huko kwa kipindi chote cha maisha yao, kisha kila baada ya miaka miwili kundi jingine la watu litakuwa likienda kwenye makazi hayo.
Ikiwa inafananishwa na Big Brother, tayari mradi huo umepata baraka za kutosha kutoka kwa wadau wanaojihusisha na mambo ya anga kutoka nchi  mbali mbali duniani. Ambao watachangia vifaa vya ujenzi na kutoa mchango wa kitaalama pale itapohitajika. Ni mradi binafsi ambao hautegemeai pesa za walipa kodi kwa hiyo haitegemewi kutokea mifarakano yoyote au kusitishwa kwa  sababu za kisiasa au hila za wanasiasa.

Muazilishi wa mradi huo ndugu Bas Lansdorp, anatazamia kutumia mbinu ya kisasa. Ujenzi wa makazi hayo utakuwa ukirushwa hewani moja kwa moja na kutoa nafasi ya kila mmoja kuweza kuushuhudia ukiendelea.
Video ya Mars one imeshapata zaidi ya watazamaji 232, 000 tangu iliporushwa kwenye youtube,com
Tayari baadhi ya wanasayansi waliobobea wameanza kuonesha shaka juu ya mradi huo, kwamba upo kinadharia zaidi.
Kwa mujibu wa mtandao Mars one kuanzia mwakani wataanza uteuzi wa wana anga watakaoshiriki kwenye mradi huo

No comments:

Post a Comment