Wednesday, 6 June 2012

Mabilionea Vijana Duniani


Mabilionea wanne vijana wanahusika moja kwa moja na facebook, wawili ni watoto wa aliyekuwa Waziri mkuu wa Lebanon Hayati Rafic Hariri, na mmoja ni mwananke. Wafuatao ni mabilionea  vijana kwa mujibu wa mtandao wa peekyou.com

1. Mark Zuckerberg
Mark Zuckerberg ambaye sasa anaumri wa miaka 28, alizindua facebook kwenye bweni lake kipindi anasoma chuo na amekuwa huku akizungukwa na wafanyabiashara wenye mafanikio makubwa duniani. Utajiri umeongezeka kwa kasi baada ya kuiorodhesha facebook kwenye soko la hisa, anathamani ya dola bilioni 15 kwa mujibu wa takwimu. Ndiye anaengoza katika orodha ya mabilionea vijana.

2. Scott Duncan
Sasa akikaribia umri wa umri wa miaka 30, amejipatia utajri wake kwa kuridhi mali kutoka kwa marehemu mzee wake, ambaye alianzisha kampuni ya Energy. Anasadikika kuwa na thamani ya dola bilioni 4 za kimarekani

3. Dustin Moskovitz
Moskovitz alifahamina na Mark tangu wapo chuoni, alifanya kazi Facebook kipindi  cha awali cha ukuaji wa kampuni ya facebook, Hivi karibuni ameamua kujihusisha na michakato mingine ikiwemo na shuhuli za misaada, kwa mujibu wa forbes anathamani ya dola bilioni 3.5



4.Sean Parker
Muanzilishi wa Kampuni ya Napster na raisi wa kwanza wa Facebook anathamani ya zaidi dola bilioni mbili. Parker mwenye umri wa miaka 32, amekuwa mshauri mkuu wa zuckerberg na ndiye anayefahamika zaidi kwa kumshauri Mark kubadilisha jina la kampuni ya facebook kutoka kwenye kuitwa “ the facebook” hadi “facebook”. Na ndiye aliyekuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kuwekeza kwenye mtandao wa muziki wa Spotify

5. Eduardo Saverin
Ni mwanzilishi mwenza wa facebook ambaye sasa anamakadirio wa utajiri wenye thamani ya dola bilioni 2, ila ilimlazimu kupigania hadhi yake hiyo, aliishitaki kampuni ya facebook, yalifanyika maelewano nje ya mahakama. Kama ilivyo wasilishwa kwenye filamu ya "The social Network", Saverin mwenye umri wa miaka 30, amekulia kwenye familia ya kitajiri anafahamika kama mpenda kula  bata.

Wengineo ni pamoja na ...
Fahdi Hariri
Robert Pera
Ayman Hariri
Yang Huiyan
Albert Von Thurn Und Taxis

No comments:

Post a Comment