![]() |
| Van Damme na Bintiye Bianca |
Maisha ya
kimapenzi ya mwana sinema mashuhuri van Damme, yamekuwa ni yenye kupendeza miaka
ya hivi karibuni, ikiwa amewahi kuoa mara tano, na kumuoa mmoja ya wake zake
hao mara mbili. Kwa minajiri hiyo inakuwa vigumu kuotea ni nani ataye ambatana
naye katika shuhuli kama hii kama mwenza wake katika tafrija kubwa kubwa kama hii.
Ila katika tuzo
za MTV jumapili hii iliyopita aliambatana na Bintiye mwenye umri wa miaka 21.
Van Damme aliongozana na bintiye Bianca Bree (jina halisi: Bianca
Van Varenberg, ambalo ni jina lake mwisho Van Damme's ). Van damme ambaye ni nyota wa
filamu ya expendables 2, alipozi na bintiye kwa ajili ya picha ya picha mbali
mbli, huku kimwana huyo akiwa amevalia
kivazi kilichovutia hisia za wengi,
Bianca
aliandika kwenye ukurasa wake wa twita kuhusiana na usiku huo “kama ambavyo
sipendi kuuza sura, ila nilipata wakati mzuri sana ” alifurahi mno kumuona Charlie sheen. Na
akiendelea kumulezea nyota huyo wa filamu ya “ Anger Management” “ni mwenye muonekano mzuri na ninampenda sana huyu jamaa kwa
lolote lile”.
Bianca amekuwa
akitokea katika filamu za baba yake tangu mwaka 2008, na kuna filamu tatu
zinafata ikiwemo “ welcome to the jungle” ambaye yupo na kaka yake Kristopher
Van Damme mwenye umri wa miaka 24. wote wakiwa ni watoto wa Van Damme na
aliyekuwa mkewe mtunisha misuli Gladys Portugues waliofunga ndoa 1987-1992 na
kuja kufunga ndoa tena mwaka 1999, ingawa Bianca anajaribu kufata njia yake
binafsi tofauti na muelekeo wa familia yake.
.jpg)
No comments:
Post a Comment