Ni ujumbe
wa twita, uliozua mijadala kwenye mitandao ya intaneti kwa kushutumiwa kuwa
unamdhalilisha mwanamke. Kampuni ya Electronics Asus iliufuta ujumbe wake huo ulioambatanishwa
na picha inayomuonyesha mwanamke akielezea bidhaa mpya ya kampuni hiyo mara tu
baada malalamiko kuanza.
Ni
picha iliopigwa kwa kuuchukua upande wa nyuma ya mwili wa mrembo huyo ikiambatana
na ujumbe unaosema “ picha ya nyuma ni nzuri sana ,
kama
ilivyo Transformer AIO”
Posti hiyo ilipotea
kwa haraka sana, ila walichelewa kwani ilishadakwa na watu kuanza kuichangia na
wenzao, na kusambaa kwa kasi kwenye mitandao mingine na malalamiko na shutuma kuanza kuelekezwa kwa
kampuni hiyo.hata hivyo kampuni ya Asus iliomba radhi kwa tukio lake hilo, na
kuahidi kuchukua hatua ambazo zitahakikisha kosa hilo halitojitokeza tena
Utamadani
wa kuwatumia wanawake warembo kwenye maonyesho ya bidhaa, umekuwa ni utaratibu
wa wakawaida kwa makampuni ya elektroniki duniani. Ila tahadhari itumike, na
kwa uangalifu wa karibu zaidi, aliongezea Bi susan Friedmann mtaalamu wa
maswala ya ya biashara kwa kusema “ nilazima uzingatie unapofanya maonyesho
kama haya, kinachoweza kukufunga Paducah yaweza kuwa sawa na Tokyo”

No comments:
Post a Comment