Meya wa jiji la new york Ndugu Michael
Bloomberg ambaye ni mrithi wa aliyekuwa meya wa jiji hilo kabla yake Bi Hillary
Clinton amelaumiwa kwa kitendo chake cha kupendekeza soda zipigwe marufuku kwa
kile kinachosemenaka kuwa zina mazara kiafya.pendekezo lake hilo limeonekana
kuwa ni laki mabavu na lina pingana na sera ya "uhuru" ya nchini marekani. Je ni
kweli soda ni hatari kwa afya yako?
Soda na tatizo la
uzito wa mwili.
Karibia asilimia 66 ya wamarekani
wanatatizo la kuwa na unene na uzito wa kupindukia.Ripoti iliotolewa na Chuo cha
Afya ya JAmii cha Harvard nchini marekanai, imeonesha kuwa kuna uhusiano mkubwa
kati ya unwaji na soda na ongezeko la uzito mwilini.Soda inachangia asimia saba
ya wastani wa kalori zinazoingia miilini kwetu kwa kila siku.Kalori za kwenye
soda zinaonekana nyepesi kulinganisha na kalori za kwenye chakula cha kawaida,
kwa kuwa chakula kitatufanya tushibe ila soda ni kimiminika, ambapo kalori zilizomo
kwenye soda zitafyonzwa na kuingia katika mfumo wetu wa chakula pasi na
kujisikia kushiba.Soda moja kwa siku yaweza changia ongezeko la hadi kilo 6.2
na mafuta mwilini kwa mwaka.
Soda na Magonjwa sugu
Soda ni sawa na dampo la sukari,
iliyokatika mfumo wa fruktos.Kopo moja la soda ni sawa na vijiko vya chai kumi vya sukari.Kitengo c ha Afya ya moyo
marekani ili kuepusha madhara ya sukari kimeshauri mtu mzima kunywa chini ya
vijiko sita vya sukari kwa siku, watoto visizidi vitatu, ila vijana walio wengi
wanakunywa hadi vijiko 34 vya sukari kwa siku kutokana na kunywa vinywaji vitamu
mara kwa mara.
Kubugia soda ya
changia ongezeko la sukari kwenye damu, kwa kipindi fulani hii yaweza kuwa sababu ya maradhi kama kisukari, moyo, na pengine
kansa.watafiti wakaendelea kusema asilimia 50 ya wanaotumia walau gramu 31 ya
soda kila siku wana hatari ya kuugua maradhi ya dizaini hii, moja ya sababu
inayoweza pelekea maradhi kwama stroku, kisukari na kusinyaa kwa mishipa ya
damu.
Hii inaashiria ongezeko la unywaji wa
soda kwa watu wazima itapelekea ongezeko la maradhaki haya katika miongo ijayo.
Soda na afya ya mifupa.
Tatizo jingine kwa vijana ni tatizo la afya ya mifupa, kama
ilivyozoeleka kwa vijana na hasa watoto kupenda kunywa soda na vinywaji vitamu
kwa wingi, na kunywa maziwa kwa uchache
Maziwa yana madini ya calcium, madini muhimu katika ukomavu wa mifupa, kama ilivyo kwa protini na virutubisho vingine vilivyomo
kwenye maziwa.soda ina madini ya fosfeti., madini ambayo yanaweza athiri ujazo
wa mifupa. Iwapo itaingia mwilini kwa
wingi kulinganisha na kiwango cha calcium. Tafiti zimethitisha kuna uhusiano wa
karibu baina ya unywaji wa soda na tatizo la mifupa kwa wanawake watu wa wazima.
Soda na Kuoza kwa meno
Umakini umeelekezwa sana kwenye uhusiano wa soda na ongezeko la
uzito mwilini. Uhusiano wa soda na athari zake kwa meno halijatazamiwa kwa
kutosha.athari iliyopo haitokani tuu na sukari iliopo kwenye soda, bali hata
kemikali zilizomo kwenye vinywaji vitamu, vya weza changia uharibifu wa meno
kwa fujo.
Ni juu yetu kupima uzito wa maelezo
haya katika kuamua kwamba soda inafaida kwetu au laa, ingawa zipo soda ambazo
hazina sukari, Diebetic soda. Changamoto inabakia kwa serikali yetu na sisi wenyewe
No comments:
Post a Comment