Wednesday, 23 May 2012

Sunglasses/Miwani ya JUA


Sunglasses za ukweli kamwe hazipitwi na wakati,  ila ni nani ambaye hajawahi kujichanganya na kuangukia kwenye suglasses za gharama, au za offer mwisho wa siku tunajikuta kuwa hazitupendezi au haziendani na muonekano wetu. Kitu cha msingi katika uchaguzi wa sunglasss nzuri, ni umbo la uso wako, kufanya shopping kwa utulivu na kwa muda wa kutosha, au kupata dondoo kadhaa, ni vigumu kujitambua wewe kama wewe ni vyema ukiambatana na mtu ili uweze kupata mtazamo wa upande wa pili

Aina nzuri au muundo mzuri wa sunglasses utategemeana na umbo la uso wako, ila ni vyema kufikiria na rangi na umbo ya fremu hayo miwani pia, mfano fremu za rangi nyeusi zinaweza zisimechi na mirindimo ya baadhi ya rangi ya ngozi.

Nunua Sunglasses za gharama kidogo, epukana na miwani ya bei rahisi, hasa ya wamachinga, sana sana zitakuacha na alama kwenye pua, au kutokukinga na miyale ya jua kama ina vyostahiki, kutana na dondoo kadhaa zitakazo kusaidia kuchagua sunglasses nzuri

Uso wenye Duara
Kama una wa babyface, mashavu yaliyojaa na kidevu cha duara, na kama unataka uso mwenye msisitizo au uso mrefu, badala ya uso laini au mpana, basi vaa sunglasses zenye fremu zilizo chongoka, kisha jiepushe sana na sunglasses zenye lens kubwa sana na zenye kinarefu , zitaficha uso wako, na kuufanya uso kuonekana mdogo.


Umbo la Moyo
Kama unakomwe pana na mashavu yenye kuchongoka Fulani, muonekano wa namna hii hufanya kidevu kuonekana kidogo, kubalance uso na kuufanya uonekane mzito, vaa sunglasses zenye umbo la mraba au fremu za duara, kisha epusha fremu ambazo ni pana sana juu kuliko chini.
Rihanna na kate Moss nyuso zao zina muonekano huu

Umbo la mraba
Kuna nyuso flani zinakama muonekano wa mraba na uso mpana, hapa unatazamia kuongeza urefu wa uso, na kufifisha engo za kidevu, fremu zenye shepu ya tufe au duara zitafifisha uso wako, kwa hiyo epusha fremu zilizochongoka na zenye ncha. Fremu nyembamba na ndogo ni chaguo zuri zitaufanya uso mdogo kuonekana mrefu. Mfano ni  gwiji wa filamu wa nchini Marekani Cameron Diaz

Uso Mrefu
Kama una uso mrefu, mwembamba, chagua fremu pana, na zenye lens kubwa kuufupisha uso.Fremu zenye muunganiko wachini unaounganisha pande mbili za uso zinavutia kwa wenye pua ndefu kuliko muunganiko zenye muunganiko mrefu, namaanisha kwa kwenda juu

Umbo la Tufe
Kama ilivyo mikato ya nywele, sura zenye umbo la tufe zinaendana na staili nyingi, za sunglasses, onyesha urembo wako halisi kwa kuvaa sunglasses zenye fremu zenye upana sawa na sehemu pana za uso wako.

No comments:

Post a Comment