Tuesday, 22 May 2012


How to look good in every photo

Jinsi ya kutoka bomba katika kila picha
Angalia kulia.
Utafiti wa kimarekani chini ya chuo cha Wake Forest University umethihirisha kuwa upande wa kushoto  wa sura una mvuto kuliko upande wa kulia,  kwa hoja kwamba sehemu hiyo ya uso huonyesha hisia . Ili kupata picha nzuri ya profile, angalia kidogo upande wa kulia ili kudhihriisha uzuro wako. , hii yaweza kutoa taswira ya sura nyembaba kwa wale wenye wenye uso wa duara
Pangilia vipodozi vyako
Kupata uso wenye mvuto,  epusha faundeshen zenye madini ya titanium.ingawa faundesheni, zinafaida kubwa katika muonekana wa kila siku, flash ya kamera, yaweza kuubadilisha muonekano kuwa wenye kutisha wenye wingu wa rangi nyeupe,  ukishapaka faundesheni yako malizia kwa kupaka  poda ya uso kupunguza mngao.
Jitokeze.
Kuhakikisha unatoka bomba kwenye picha , hakiksha unasisitiza na kuonyesha sehemu zako zenye mvuto zinaonekana kimvuto , jaribu kupaka eyeline. Tofauti na hapo paka lipstick kwa mbali , kasha vaa nguo mbayo inayoendana na rangi ya ngozi yako, na shepu yake
Usitazame Lens Moja kwa Moja.
Hakuna anayetaka macho ya kusinzia au mekundu , huaribu picha nzuri, hakikisha unaepusha hii hali kwa kukwepesha macho kwenye kamera , kwa kuangalia chini au juu ya camera. Kuangalia moja kwa moja kwenye lens itapelekea mwanga wa flash ya kamera kufanya mboni ya macho kuwa mekundu, kwepesha macho ili usikutane na macho kuwa yamesinzia sababu ya kuya kwapua
Epusha Macho mekundu.(red eye).
Macho kuwa mekundu kwenye picha husababishwa na reflecting kutoka nyuma ya macho, wale wenye mboni kubwa,wana uwezekano mkubwa wa kupatwa nah ii halii.kama kukwepesha macho haisadii basi jaribu kuhakikisha hilo eneo lina mwangaza wa kutosha, au wewe kuwa na nuru ya kutosha kabla ya kupiga or  au angalia mwangaza ili mboni za macho yako ziwe ndogo
Epusha mwanga wa moja kwa moja
Inaweza shindikana kuudhibiti moja kwa moja mwanga wa kamera yako, labda uwe mwana mitindo uliyebobea. ila ni vizuri kutambua kuwa mwangaza wa moja kkwa moja toka juu waweza pelekea vivuli usoni mwako, na kuaribu muonekano wako, chagua maeneo yenye mwangaza mwepesi,  au nenda kwenye kivuli kama ni nje
Pozi kama profeshono.
Kama ni picha ya mwili mzima, lifanyie mazoezi kwa  muda mrefu pozi lako, kwa kuzungusha mwili wako robo tatu kwa kuelekea kamera , huku bega moja likielekea camera huku mguu mmoja ukiwa mbele ya mwenzake.itafanya mwili wako  uonekane mwembamba, kuliko,jaribu kurudisha mgongo wako na bega lako nyuma, tumbo lako kwa ndani. Kidogo vuta hewa ndani.
Tambua tabasamu zuri.
Wengi huelekeza umakini wetu kwenye midomo tunapotaka kutabasamu, ila kwa mujibu wa mwana  mitindo mashuhuri Tyra banks, ni jinsi ya kutawamu kwa macho, kuliko kulazimisha tabasamu , jaribu kufikiria vuta hisia ya kitu ambacho kitakufanya ufurahi, ili kupata tabasamu halisia, unaweza kulipendezesha tabasamu lako kwa kuzingatia viungo vyako,
kwa mfano, tabasamu pana kwa wale wenye meno mazuri, au tabasamu fupi, hupelekea macho kuonekana madogo na yenye mvuto.

Pozi..
Fanyia mazoezi pozi lako,
Kama kweli upo makini kupata picha nzuri, kitu kizuri na chamsingi ni kuhakikisha kuwa unajipanga ila kupata pozi zuri, fanyia mazoezi kwa sura na engo tofatu za mwili, tabasamu, ili kupata muonekano mzuri unaondendana na wewe, iwe mbele ya kamera au kwa kutumia kamera yako wewe mwenywe. Ukwisha gundua nini kinakupendeza wewe, basi hakikisha unatoka vizuri kila mara

Makala zingine

No comments:

Post a Comment