Pangilia maisha yako ya kazi
Kama shuhuli zako za
kazini zinakuacha ukiwa na mvutano wa mawazo, au unajihisi ni kama
uliyezingirwa na kuzidiwa na mambo, tambua umefika muda wa kutulia, na
kupangilia mambo yako.Kwanza hakikisha unawasili kazini japo dakika tano kabla
ya muda unaotakiwa kuripoti kazini, utaratibu huu utakupa muda wa kupanga
majukumu yako ya siku hiyo, na kujituliza kisaikolojia vile vile.
Pili tenga nafasi ya
kutosha ya kufanyia kazi, kwa kutoa vitu vilivyozagaa mezani, au eneo lako la
kufanyia kazi kwa ujumle, pamoja na kufuta email za zamani ambazo hazina
umuhimu, pitia email za kwenye scam japo kwa juuu huwezi jua panaweza kuwa na
ujumbe wa muhimu kasha ndio uzifute fanya hivi mara kwa mara ili zisiwe nyingi
ukajikuta huwezi kuzithibiti ipasavyo. Kasha andaa orodha ya mambo ambayo
utahitajika kufanya kwa siku hiyo, fanya hivyo kwa kuzingatia kipaunmbele. Ukiweza
jaribu kuanza na kazi ngumu, ilikuondoa mzigo wa mawazo kichwani mwako.
Vaa vazi litakalo ibua mudi yako
Ilhali wengine wetu
tunalazamika kuvaa uniform za kazini au mpangilio Fulani wa nguo unaokubalika
kazini, kama una uhuru wa kutosha yaani hamjawekewa vikwazo vya nguo aina gani za
kuvaa, chagua nguo au vikolombwezo vitakavyo kupa uchangamfu, kama utavaa mikufu
itakayokuletea kumbukumbu nzuri, begi zuri lenye rangi nzuri litakalo angazia
siku yako, au vazi ambalo litakokuza kujiamini kwako, au hata nguo yako ya
ndani, vaa vazi ambalo litaangazia siku yako na kukufanya uwe mwenye furaha
Badilisha Mpangilio wako wa
kazi
Kuwa mienendo yako sio
lazima kila mara uwe unafata utaratibu ule ule, katika maisha yako ya kazi ya
kila siku, kufata utaratibu huo huo kila siku itakufanya ujisikie ni mwenye
kukosa mizuka. Kwa hiyo jaribu kitu kipya au utaritibu mpya kila inapowezekana
kwa namna yoyote unavyoweza.Fanya kazi za kila siku katika mpangilio mwingine,
kuongea na mtu ambaye hukuwahi zungumza naye hapo kabla, au hata kutumia usafiri wa aina tofauti, kama baiskeli. Kama
umeshindwa kabisa kubadilisha mpangilio wako wa kazi basi , jaribu kitu kizuri,
cha kusisimua na tofauti wakati wa chakula cha mchana aua wakati wa mapumziko.
Ongeza nuru mezani kwako
Utafiti
unaonyesha kuwa wafanyakazi waliochukua muda kungarisha au kuweka athari kwenye
meza au eneo lao la kazi, basi wanauwezekano mkubwa wa kuwa na furaha asilimia 40 ya furaha
kulinganisha na wenzao. Inawezekana ukakosa idhini au mamlaka ya kuremba eneo
lako la kazi, ila kama unaweza basi pangilia ofisi yako au eneo lako la kazi,
kwa kununua vitu binafsi, kama vya steshonari,
picha ya sherehe Fulani hivi, kalenda ya kuchekesha au kitu cha sanaa, au hata
mmea, mazingira mazuri yenye kuvutia ni lazima yata kuchan
Changamka kazini
Kama kazi yako
inakuboa, jaribu kujichangamsha, kwa kujipa viji zoezi kipindi cha mapumziko ya
chakula cha mchana.mazoezi ni mazuri kwa kukuchangamsha, huongeza kujiamini
kwako, na kupoteza mvutano wa mawazo, na vile vile inapelekea ubongo kuachia
aina Fulani ya kemikali iitwayo endorphins na anandamide ambazo zaweza
kukuchamngamsha na kukuacha mwenye kujisikia furaha, na huru. Kama kuna bafu,
basi pata shawa, au tembea tembea kama ni
madukani kuchangamsha mapigo yako ya moyo, na hutokuwa na haja ya kuoga.
Tafuna tafuna vitafunwa
Je unasiku ngumu
mbeleni? basi hakikisha umepaka vitu vizuri kwenye begi lako unapoenda kazini,
vitakuongezea nguvu, vitu kama vya sukari sukari, na kukuchangamsha vile
vile.baadhi ya virutubisho kwenye chakula vya weza kuchangia namna ambavyo
unajisikia, vyakula kama ndizi, vyakula vya
nafaka.
Kuwa positive/chanya na mchangamfu kwa
wenzako.
Bila kujali namna
ambavyo unajisikia, jaribu kuwa mchangafu kwa wenzako, hata wale ambao
wanakukera na kukuchefua mno.Jaribu
kusuluhisha migogoro, epusha umbea, na
mtendee wema kila mmoja pasi na kubagua, utafiti unaonyesha kitendo cha
kutabasamu yaweza kukufanya uwe na furaha zaidi, kwa hio jaribu kulazimisha
tabasamu
Ridhika kwa kuwa unakazi
No comments:
Post a Comment