Thursday, 24 May 2012

Raisi Bill Clinton apiga Picha na wacheza filamu za Ngono


Kuna picha zimekuwa zikizagaa kwenye mitandao zinazomuonyesha Raisi wa zamani wa Taifa kubwa ulimwengu Bill Clinton akipiga picha na Wacheza filamu za ngono, maarufu nchini marekani….Picha hizo zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao pengine utakuwa umejiuliza mke wake Bi Hillary Clinton amejisikiaje au atachukua hatua gani kutokana na picha hizo., kwa kuzingatia historia ya mume wake na aliyekuwa msaidizi wake kipindi hicho yupo madarakani Bi Lewisky.
Pamoja kwamba wamevaa nguo, ila hata hivyo imekuwa gumzo hasa kwa magazeti ya udaku.

Picha hiyo imepigwa katika shuhuli iliondaliwa na Raisi huyo pamoja na Mtoto wa mfalme wa Monaco, bwana Albert wa Monaco, ili kuisaida kituo cha misaada cha William J. Clinton. Pengine unajiuliza kwa nini pawe na wacheza filamu za ngono, kimsingi haijafahamika.palikuwa na nyota wengine, ila picha pekee iliopatikana kutokana na hii shuhuli ni ya raisi Clinton na wachezaji filamu hao, Brooklyn Lee wa Secretaries 4( na ndiye aliye twit hiyo picha), na upande mwingine yupo Tasha Reign , wa filamu za mvuto Farm Girls Gone Bad, wa mwisho aliktambulika kama Jennifer Taule @jennifer_taule.

Pengine hapa tunapata picha gani, wanablog wengi wamekuwa wakijoki, je Bill Clinton alifahamu wasifu wa hawa mabinti ?
Magazeti ya udaku, ya uingereza si cha kushangaza ya kiifafanua hii habari kama ni yenye kusikitisha, yenye kukumbushia machungu ya miaka iliopita, hasa kwa kuzingatia historia yake na Monica Lewisky, na kuongezea aina ya mwanamke kama BI Hillary Clinton, kila dalili zinaonyesha kuwa bingwa atakuwa anabanwa sasa hivi kwa kitendo chake hicho cha kupiga picha na mabiti hao

Ila hata hivyo ni kichekesho ila si kichekesho cha kubeza, kwa kujaribu kuhusianisha picha nzima, vicheko na kumbukumbu zilizopita, na tukio la Bi Hillary Clinton akinywa bia Cartagena, au picha ya tukio la hivi karibuni linamuonesha Bi Hillary Clinton akijipaka lipstick akiwa kazini wakati wa kazi. Wadau walihitimisha kwa kuoneshwa kuchukizwa kwao na  picha hizi na kumkebehi kwa  kudai kuwa hana mvuto, si mwenye kuzingatia majukumu yake, na ni fedheha kwa uanamke wake.je unadhani kuwa Hillary atashtushwa na picha hizi kwa tathmini na muonekano wa mienendo yake.

Pengine vile vile yupo bize sana na majukumu ya kazi, kiasi cha yeye kukosa muda wa kushuhulishwa na vimbanga hv

No comments:

Post a Comment