Saturday, 26 May 2012

Abramovich ategemea kumpa Dimatteo mwaka mmoja wa majaribio.


MMiliki huyo mwenye asili ya urusi bado hajaridhishwa na utendaji wa kocha huyo Mitaliano, achilia mbali mafanikio aliyoyapata kwa kufanikiwa kuchukua kombe la fa, na klabu bingwa ulaya UEFA msimu huu


Mmiliki wa  team ya Chelsea asemekena atamkabidhi mkataba wa mwaka mmoja, baada ya bado kujikuta hajashawishika na uwezo wake kwa mujibu wa The times
Tangu kuchaguliwa kwake kwa kipindi cha mpito, kufatia kufukuzwa kasi kwa aliyekuwa kocha wa zamani Andre Villas Boas, ameibeab team hiyo , na kuipa mataji matukufu
Na ikiwa bado Abramovich hamuoni kama kocha mwenye hadhi ya juu, amekubali kuwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 41, anastahiki kupewa nafasi nyingine katika uwanja wa Stamford Bridge, baada ya kumpa mafanikio ya hali ya juu msimu huu
Hata hivyo maamuzi yeyote yanaweza kufikiwa hadi wiki ijayo, ikimaanisha  kuwa midifilda huyo wa zamani anaweza kwenda mapumziko mafupi kabla ya hatma yake kuamauliwa
Pamoja na kwamba muitaliano huyo ana kingiwa kifua, na kikosi cha klabu hiyo , pamoja na wapenzi wa timu hiyo , bado mmiliki  huyo anamatumaini ya kuweza kumshawishi Pep Guardiola kuja Lomdon, baada ya ya kocha huyo kutangaza kuachia ngazi kwenye timu yake ya Barcelona

No comments:

Post a Comment