Ushindi mnono wa timu ya Chelsea jumamosi hii, umehitimisha ndoto ya muda mrefu wa mmiliki wa timu hiyo bwana Abramovich.
Gwiji huyu msiri wa biashara za mafuta amekuwa akiyafukuzia mafanikio hayo kwa kipindi cha muda mrefu sasa tangu mwaka 2003, timu ya Chelsea yenye makazi yake jijini London , lilipata ushindi huo mwembamba kwa kupitia mcheza wake Didie Drogba, ambaye hadi sasa haileweki kama atabaki kuchezea timu hiyo msimu ujao au laa.
Mafanikio ya ndugu Abramovich mwenye umri wa miaka 45,sasa hayakuja kirahisi, nibaada ya kutumia kiwango kikubwa cha pesa, katika kusajili wachezaji, mishahara matengenezo ya miundombinu ya klabu katika kufukuzia utukufu huo wa bara ya ulaya.
Abramovich aliifufua timu hiyo, iliyokuwa katika hali ngumu ya kiuchumi, na kuibadilisha kuwa tishio barani ulaya, ambapo katika uangalizi wake amenunua idadi ya wachezaji 66, ya wachezaji mashuhuri na wagharama duniani,
No comments:
Post a Comment