Wanawake
walio wengi katika kipindi cha maisha yao
huvaa viatu virefu, huvaliwa kuongeza urembo, huifanya miguu, ivutie, kuonekana
mirefu miembamba na yenye mvuto.na upande mwingine wanaume huvutiwa na wanawake
wanapokuwa wamevaa viatu virefu

Kwa wengine wetu viatu virefu ni sehemu ya
maisha yetu ya kila siku, huvaa tuendapo ofisini, tunapokuwa kwenye matembezi
ya mwisho ya wiki, mitoko ya jioni, au katika shuhuli maalum, hayo yote ni kwa
ajili tuu ya kuonekana warembo. Kwa nini usijihusishe na viatu ambavyo ambavyo
vitavuka matetegemeo yako
Miaka iliyopita nilikuwa na viatu virefu vizuri na vibaya.
kuna viatu virefu vya aina tofatuti madukani, virefu sana , vyembamba chini ya nchi mbili, na
vyenye unene wa nchi 0.4.
Kuna faida nyingi ya
kuvaa aina hii ya viatu, inaulazimisha mwili kuweza kuzunguka, inafanya
muonekana wa makalio na matiti kuvutia, muonekano wa mwanamke wa kisasa.
Hufanya visigino kuonekana vidogo, hufanya mifupa
inayotengeneza unyayo kuwa mirefu kuinuka na yenye kuleta maana zaidi.
hupelekea mkao(posture) ya mvaaji kutulia kitu ambacho husaidi uti wa mgongo.
Nina urefu wa nchi
5’5” sio mrefu wala mrefu, nipo katikati.ila tayari ninayo miguu mirefu, ninapo
vivaa viatu urefu wangu huongezeka hadi kufikia 5’7”.Viatu vyangu virefu huwa
kwenye maboksi yake kabatini.huwa navaa, kwa mitoko ya usiku, maharusi na
wakati mwingine ili tuu niwe na muonekano wa
miguu mirefu.
Style yangu kifashen
hubadilika mara kwa mara hujikuta na vaa viatu vye muonekano tofauti kwa
madhumuni tofauti, hupenda sehemu ya chini ya miguu yangu ionekane hasa pale,
ninapovaa nguo simple, viatu vyangu
hunitoa moja kwa moja na kunijengea kujiamini.
Najua kuwa mara kadhaa vaitu virefu huu miza miguu, hata mimi imewahi
kunitokea, Hizi ndio nyenzo zangu ambazo hutumia, na pengine itapelekea viatu
vyako hivyo vya gharama kukunufaisha
Nunua kiatu cha saizi yako: bila shaka hii inaonekana kuwa ni kitu
cha kawaida, ila lini ilikuwa mara ya mwisho kwako kwenda dukani kwa ajili ya
kupima urefu wa miguu yako.Wataalamu wanaamini kuwa miguu huongezeka urefu
kadri siku zainavyokwenda, na ujauzito huweza pelekea urefu wa unyayo wa mguu kuongezeka
vile vile. ndio maana ni muhimu kupima urefu wa miguu yako, kila unapo enda
kununua viatu.hakikisha hakuna nafasi iliobakia yenye urefu sawa na kidole
gumba kati ya kidole chako kirefu cha miguuni na mwisho wa kiatu, kwa viatu
virefu ni muhimu kufanya hivi ili uweze kustarehe pale utapo vivaa.
Vaa vyenye uduara
Tumebahatika kwa kuwa
viatu vya duara huwa havitoki kwenye fasheni ukilinganisha na vilivyo chongeka
mbele, vilivyo chongeka vyaweza kukupeleka kupindisha kidole chako kirefu kwa
ndani, chanzo cha maumivu ya vidole, na hata kupata sugu vidoleni, ilhali viatu
vyenye uduara mishoni hukupa nafasi ya kunyoosha vidole vyako.iwapo huwezi
kuachana kabisa na viatu virefu basi
basi kuwa na vya uduara ili kubadilisha pale itapokulazimu.
Tambua unene wa kiatu.
Wakati mwinginie
vidole sio tatizo, zingatia unene wa kiatu.viatu vingi vya fasheni huja katika
unene wa kawaida, ila kama una nyayo nene,
unene wa kawaida utakupa shida. Unapokutana na kiatu kinachokuvutia, angalia kama
kuna kingine chake ambacho unene wake unaendana na wewe, kama
sivyo basi mafundi viatu huweza kuvinyoosha na na kuongeza komfotability.
Vijaze nyama.
Baada ya kuzingatia
kuwa viatu hivyo havikubani, sasa ni wakati wa kuangalia kama
vina nyama kutosha.mara nyingi visigino na unyayo kwa ujumla huuma kwa sababu
ya maumivu yatokanayo na kitako cha viatu, jaribu kutafuta namna ya kupunguza maumivu
hayo
Kiatu mbadala
Kuvaa viatu virefu kwa muda mrefu, huweza
kukufanya ujisikie kama nyayo zako
zimeinuka.Ili kuendeleza comfort , jenga utaratibu wa kuvaa viatu vya kawadia.
Ingawa viatu virefu, hukuza urefu wa miguu yako, havina umuhimu sana pale unapovaa
suruali, kwa hio upe unyayo wako mapumziko.
Tunnza nyayo za miguu yako.
Hakuna kinacho haribu
muonekano wa viatu virefu kama unyayo usio na mvuto, kama
unamalengo ya kuonesha vikuku vya miguuni, basi wekeza kwenye pedicure angalau
kila wiki.
Inachukua muda kuzoea
viatu virefu , ila kuwa na viatu vyako vya kawaida iwapo lolote likijitokeza, tembea na plasta
huwezi jua michubuko yaweza kujitokeza wakati gani.
Kwa kuhitimisha, tafadhali tunza miguu yako, viatu virefu
vinapendeza na kila mtu anavipenda
“sijui ni nani aliyegundua viatu ila kila mwanamke ana deni
kwake”marilyn Monroe
Makala zingine
http://kipepe-sikika.blogspot.co.uk/2012/05/sababu-halisi-inayokufanya-uwena-uchovu.html
http://kipepe-sikika.blogspot.co.uk/2012/05/sababu-halisi-inayokufanya-uwena-uchovu.html
No comments:
Post a Comment